Ni ipi sababu ya Rais Samia kuwa karibu sana na kuipa uzito Nchi ya Oman?

Ni ipi sababu ya Rais Samia kuwa karibu sana na kuipa uzito Nchi ya Oman?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Nimekuwa nikiona Rais wetu akiipa uzito hii nchi ya kuitwa Oman.

Hadi sasa ninachojua tu ni kwamba Zanzibar ilikuwa koloni la Oman na masultani wake walikuwa na asili ya Oman.

Ila leo pia nimeona hii nchi nayo ipo mbioni katika kinyanganyiro cha kujenga Bandari ya Bagamoyo.

Kwa anaejua japo hata kidogo ningependa kujua nini hasa kipo nyuma ya pazia.
 
Znz chini ya sultani, ilikuwa koloni la Oman miaka mingii, so wazenji wengi mahaba yao yapo huko

Hawa waZenj wamepumbazwa sana na vijizawadi wanavyopewa kutoka kwa watawala wa Oman ambao ni ndugu wa Sultan aliyepinduliwa 1964!!

Sijui kwanini wanadhani hawa waliopinduliwa na sasa wako Oman hawataki kurudisha kile ambacho wanaamini walinyang'anywa? Mimi naona wanakula timing tu siku moja mtakuja kukuta manowali iko nje ya Bandari wanayojenga na hapo ndiyo mtakapojua kunyoa au kusuka?
 
Nimekuwa nikiona raisi wetu akiipa uzito hii nchi ya kuitwa Oman.

Hadi sasa ninachojua tu ni kwamba Zanzibar ilikuwa koloni la Oman na kwa sasa watawala wa Oman ni ndugu wa Sultan aliyepinduliwa 1964 kwenye mapinduzi ya Zanzibar.

Ila leo pia nimeona hii nchi nayo ipo mbioni katika kinyanganyiro cha kujenga bandari ya Bagamoyo.

Kwa anaejua japo hata kidogo ningependa kujua nini hasa kipo nyuma ya pazia.
Yaani wabongo bhana.... mbona kutwa tukiisifia USA, UK na nchi nyingi za Ulaya ambazo zilikuwa ni Wakoloni wetu na hatuoni shida????

Haya makengeza mpaka kwenye kufikiri yatatulemaza akili zetu....

Leo hii huwezi kuta familia hapa Tanzania zenye mchanganyiko wa damu kati ya wazawa na Wajerumani au Waingereza meaning walituchukulia kama watumwa na daraja la pili kwao... lakini kwa upande wa Oman ni tofauti meaning wanawaona Zanzibar kama sehemu ya ndugu zao....

KUNA UBAYA GANI WAKISHIRIKI KUWEKEZA HUMU NA KUIMARISHA MASHIRIKIANO YA KIUCHUMI?

TUACHE KUFIKIRI KINYUMENYUME JAMANI...

Oman yenye watu chini ya 10M wanaweza kweli to Overdue the Country of more than 60M? Tutakuwa mazombi siyo bure.
 
Yaani wabongo bhana.... mbona kutwa tukiisifia USA, UK na nchi nyingi za Ulaya ambazo zilikuwa ni Wakoloni wetu na hatuoni shida????

Haya makengeza mpaka kwenye kufikiri yatatulemaza akili zetu...
Hao kina Uk, Usa, France, nk ni super powers zenye influence kubwa sana.

Taabu ipi hapo kwa Oman.
 
Kutwa tunasifia makoloni yaliyotutawala....Ujerumani+ Uingereza.....

Kwanini dhambi iwe kwa hao WAOMANI?!!!

Hebu tapikeni hizo propaganda koko mlizojilisha ili ELIMU TULIYOIPATA IWE KWELI MKOMBOZI WA MWAFRIKA.....

N.B: Jamshid alikimbilia Uingereza...je hamuoni mahusiano ya dola lao na huko Uingereza kunakosifiwa na baadhi yetu?!!! Ama kwa kuwa huko Oman ni kwa watu weupe wasiokuwa WAZUNGU?!!!

#Siempre JMT🙏
#Siempre SSH🙏
 
Hao kina Uk, Usa, France, nk ni super powers zenye influence kubwa sana.

Taabu ipi hapo kwa Oman.
Unataka Ufaransa iwe na influence kubwa kwa Zanzibar kuliko Oman ?!!!

Mbona Afrika Magharibi yote kumejaa influence ya Ufaransa(lugha +utamaduni)....kwanini dhambi iwe ni kwa Zanzibar na kutakiwe kusiwe na kumbukumbu /uhusiano wowote wa hao waomani ?!!!

Hebu ziongezeeni thamani hizo elimu zenu ndogo mlizozipata.....

#Siempre JMT🙏
 
Hawa waZenj wamepumbazwa sana na vijizawadi wanavyopewa kutoka kwa watawala wa Oman ambao ni ndugu wa Sultan aliyepinduliwa 1964!! Sijui kwanini wanadhani hawa waliopinduliwa na sasa wako Oman hawataki kurudisha kile ambacho wanaamini walinyang'anywa? Mimi naona wanawakula timing tu siku moja mtakuja kukuta manowali iko nje ya Bandari wanayojenga na hapo ndiyo mtakapojua kunyoa au kusuka?
Kwanza ungejifunza historia ya Zanzibar kabla ya kutuletea hisia zako koko zilizoujaza moyo wako na zilizo kinyume na UHALISIA wa unayotaka kutufafanulia hapa.....
 
Nimekuwa nikiona raisi wetu akiipa uzito hii nchi ya kuitwa Oman.

Hadi sasa ninachojua tu ni kwamba Zanzibar ilikuwa koloni la Oman na masultani wake walikuwa na asili ya Oman...
Acha kuwa na akili potofu unakumbuka wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Waziri Mkuu Salim Ahamed Salim Tanzania ilipewa misaada mikubwa kutoka Oman.

Tatizo la watu kama wewe ni kuona Rais anatoka Zanzibar.
 
Hao kina Uk, Usa, France, nk ni super powers zenye influence kubwa sana.

Taabu ipi hapo kwa Oman.
😂😂😂😂😂😂

Tabu ni namna tunavyofikiri tu... hebu google PM wa UK wiki hii yupo ziarani wapi kama siyo kwenye nchi ambazo kwa upni wako siyo superpowers?

Usiwe short sighted na negative hivyo.... tutor muda tuione na tupinge kwa facts...
 
Mtoa mada umekurupuka na umedhihirisha jinsi ulivyo "mweupe" kichwani..

Kwa taarifa yako, mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ni ushirikiano kati ya wawekezaji wawili ambao ni Mchina na Muoman. Kama ulikuwa hujui ndio nakufahamisha, na haijaanza wakati wa Samia bali tokea mkataba wa awali.

Unakuja hapa unawazoa wajinga wenzako, na umefanikiwa sana juu ya hilo.

Mwisho namalizia kusema kwamba WaOman ni ndugu zetu na tunawapenda sana. Kama wewe unawachukia kasage chupa unywe..
 
Kwako wewe mzanzibari ni mtanzania nusu asiyestahili kuwa RAIS wa taifa hili....

Sijui ujinga +upumbavu huo ni elimu uliyofundishwa?!!

Sijui ujinga na upumbavu huo ni HISIA na matakwa mfu ya moyo wako tu ?!!!

Una matatizo....

Kamsome Kamarada Salim Ahmed Salim alipokuwa waziri mkuu na mahusiano yetu na hao Oman.....

Shida yetu baadhi ya vijana si WADADISI WA KUTANGULIZA UHALISIA ZAIDI YA HISIA ZETU KOKO TU...NI HISIA TU ZA HOVYO

N.B Tulikuwa na shida ya mafuta kipindi cha nyuma....kasome kipi kilisaidia kuyapata.....

#Siempre JMT🙏
 
Inawezekana anaanda mazingira ya hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa , upinzani ukichukua nchi.
Inawezekana pia kukawa na ndugu zake huko, kama wajomba hivi!

Pia ni kawaida sana kwa wanasiasa wetu kuwa karibu zaidi na watawala wetu (wakoloni). Kambona alipokimbia nchi hakwenda Oman, hivyo hivyo, Samia naye anaweza kukimbilia Oman kuliko kukimbilia Uingereza.
 
Kwako wewe mzanzibari ni mtanzania nusu asiyestahili kuwa RAIS wa taifa hili....

Sijui ujinga +upumbavu huo ni elimu uliyofundishwa?...🙏
Shida inaanzia kwenye shule za kata zinazalisha vijana wenye uelewa mdogo sana mambo though sio wote, vijana wa leo hawafikilii kingine zaidi ya ushabiki na mihemko ya mambo, pia mizizi ya umaskini na kutoka kwenye familia za kichawi inachangia kuwa na vijana ambao upeo wao umeegemea kwenye chuki, husda na wivu.

Angalizo, hivi sasa kuna plotting conspiracy nyingi sana ambavo zinaonekana wazi kumchonganisha Rais as an individual na wananchi wake hivyo vijana tuingalie Tanzania yetu ya kesho, tujitambue na tujue wajibu wetu kwa ajili ya taifa letu
 
Back
Top Bottom