Jagina
JF-Expert Member
- Jan 29, 2019
- 8,428
- 4,022
Tatizo letu kubwa tumegawanyika,
Wako wanaofikiri kikristo na wako wanaofikiri kiislam. Tunaofikiri kiasili tumebaki wachache sana.
Wanaofikiri kikristo wanaona Umagharibi ni Bora na kutwa kucha wanavutiwa na Kila cha magharibi kama kuvaa, lugha zao, kula kwao, vitu vyao, na kipimo cha kuendelea Ni kuwa kama wamagharibi.
Wanaofikiri kiislam wanaona Uarabu ni ustaarabu, kujua kiarabu ni kuwa jirani na Mungu. Kuvaa kanzu na barghashia ni kilele cha heshma, etc. Wanajisikia kuwa waarabu.
Tunaofikiri kiasili tunawaona wote hayo makundi mawili ni binadamu sawa na binadamu yeyote duniani. Tunaisoma historia katika jicho la mapambano. Tunaona tunahitaji kupambana zaidi ya kulalamika Kila muda. Tunaangalia fursa kokote.
Kwa ufupi. Siku nyingine nitaandika zaidi
Hiyo historia unaisoma kitabu gani cha asili?