Ni jadi ya Yanga kuchangia katika shughuli mbali mbali za kijamii, maendeleo na yote yale ya muhimu pale inapohitajika

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
23,234
Reaction score
28,473
Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans, Mzee Mangara Tabu Mangara, (mwenye kofia), alikabidhi hundi ya shilingi 10,000 kwa Mzee Omari Londo, Mwenyekiti wa TANU wa mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1974.

Fedha hizo zilikuwa ni mchango wa klabu hiyo kwa ajili ya kusaidia harakati za ukombozi wa Afrika.

Hafla hiyo fupi ilikuwa kielelezo cha mshikamano wa michezo na siasa, kwamba mpira wa miguu, hasa klabu kongwe kama Yanga na Simba, haukuwa burudani tu bali pia nyenzo ya mshikamo wa kijamii na kisiasa.

Mwaka 1974 Afrika ilikuwa bado inasaka uhuru kamili: Msumbiji na Angola walikuwa karibu kuondoa minyororo ya Wareno, Zimbabwe bado chini ya Ian Smith, na Afrika Kusini ikiwa imekumbwa na giza la ubaguzi wa rangi. Hivyo mchango wa shilingi 10,000 haukuwa fedha tu, bali ulikuwa alama ya mshikamano na mshikamano wa Afrika.
#C & P, KUTOKA KWA BWANA MICHUZI ISSA,NGULI.
Screenshot_20250819-114304~2.jpg
 
SIKU YANGA WALIPOCHANGIA SHILINGI
ELFU 10 KUSAIDIA UKOMBOZI
WA BARA LA AFRIKA

Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans, Mzee Mangara Tabu Mangara, (mwenye kofia), alikabidhi hundi ya shilingi 10,000 kwa Mzee Omari Londo, Mwenyekiti wa TANU wa mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1974.

Fedha hizo zilikuwa ni mchango wa klabu hiyo kwa ajili ya kusaidia harakati za ukombozi wa Afrika.

Hafla hiyo fupi ilikuwa kielelezo cha mshikamano wa michezo na siasa, kwamba mpira wa miguu, hasa klabu kongwe kama Yanga na Simba, haukuwa burudani tu bali pia nyenzo ya mshikamo wa kijamii na kisiasa.

Mwaka 1974 Afrika ilikuwa bado inasaka uhuru kamili: Msumbiji na Angola walikuwa karibu kuondoa minyororo ya Wareno, Zimbabwe bado chini ya Ian Smith, na Afrika Kusini ikiwa imekumbwa na giza la ubaguzi wa rangi. Hivyo mchango wa shilingi 10,000 haukuwa fedha tu, bali ulikuwa alama ya mshikamano na mshikamano wa Afrika.
#C & P, KUTOKA KWA BWANA MICHUZI ISSA,NGULI.View attachment 3446078
Duuuh aisee
 
Kuna jambo la kufikiria hapo nimepata japo ni nje ya mada...

Ina maana miaka kadhaa mbele ukimwambia mtoto wako kua enzi zetu tulikua tunahangaika kutafuta milioni Moja anaweza akakucheka.. kama ambavyo Kwa Sasa nacheka Mimi kuskia yanga kama taasisi ilichangia elfu 10 miaka ya nyuma??
 
Kwahiyo injinia topolo akiitwa akajieleze ataenda na kajipicha kwamba hatujaanza leo? Wenye akili pale ni wawili tu .
 
Umenikumbusha timu zangu pendwa Pan Africans na Nyota Nyekundu 😂

Pan Africa alikuwepo beki Mohamed Mkweche na kule Red Star alikuwepo mtemi Rosta Ndunguru

Kitambo sana bwashee 😂🙏
 
Uongozi wa Yanga umechemka kwenye hilo hawataki kukubali michezo na siasa abadani haviendani kwahiyo mashabiki wa vyama vingine wanajisikiaje huyo muhandisi wenu kachemka pakubwa sana. Nafikiri kujiona anakubalika anajaribu kujivutia kwa wanasiasa ambao kamwe sio wa kuaminika.​
 
Kuna jambo la kufikiria hapo nimepata japo ni nje ya mada...

Ina maana miaka kadhaa mbele ukimwambia mtoto wako kua enzi zetu tulikua tunahangaika kutafuta milioni Moja anaweza akakucheka.. kama ambavyo Kwa Sasa nacheka Mimi kuskia yanga kama taasisi ilichangia elfu 10 miaka ya nyuma??
Miaka ya 74, kiasi cha shs 5000/- ulikuwa unanunua nyumba mnazi mmoja,lumumba st.
 
Utopolo na maisha ya misifa ya bila kutumia akili.....tumeshawambieni mara nyingi kila jambo mnalotaka kufanya sharti muige kutoka simba mkifanya Kwa akili zenu wenyewe Wana utopolo ni lazima muharibu....
 
Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans, Mzee Mangara Tabu Mangara, (mwenye kofia), alikabidhi hundi ya shilingi 10,000 kwa Mzee Omari Londo, Mwenyekiti wa TANU wa mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1974.

Fedha hizo zilikuwa ni mchango wa klabu hiyo kwa ajili ya kusaidia harakati za ukombozi wa Afrika.

Hafla hiyo fupi ilikuwa kielelezo cha mshikamano wa michezo na siasa, kwamba mpira wa miguu, hasa klabu kongwe kama Yanga na Simba, haukuwa burudani tu bali pia nyenzo ya mshikamo wa kijamii na kisiasa.

Mwaka 1974 Afrika ilikuwa bado inasaka uhuru kamili: Msumbiji na Angola walikuwa karibu kuondoa minyororo ya Wareno, Zimbabwe bado chini ya Ian Smith, na Afrika Kusini ikiwa imekumbwa na giza la ubaguzi wa rangi. Hivyo mchango wa shilingi 10,000 haukuwa fedha tu, bali ulikuwa alama ya mshikamano na mshikamano wa Afrika.
#C & P, KUTOKA KWA BWANA MICHUZI ISSA,NGULI.View attachment 3446078
Ukisikia shughuri za kijamii si vyama vya aina yoyote vyenye muelekeo wa kundi maalumu lisilohusu baadhi ya watu, mfano makanisa, misikiti, ngoma na lolote lenye kiingilio kujiunga.
Mwaka 1974 wananchi wote tulikuwa chini ya chama cha Tanu.
 
Mawakili wa UtopwiX walivyokuwa vilaza watapeleka hizo picha ikitokea watafunguliwa file la kesi. Manara ajengewe sanamu
 
Back
Top Bottom