Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 23,234
- 28,473
Duuuh aiseeSIKU YANGA WALIPOCHANGIA SHILINGI
ELFU 10 KUSAIDIA UKOMBOZI
WA BARA LA AFRIKA
Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans, Mzee Mangara Tabu Mangara, (mwenye kofia), alikabidhi hundi ya shilingi 10,000 kwa Mzee Omari Londo, Mwenyekiti wa TANU wa mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1974.
Fedha hizo zilikuwa ni mchango wa klabu hiyo kwa ajili ya kusaidia harakati za ukombozi wa Afrika.
Hafla hiyo fupi ilikuwa kielelezo cha mshikamano wa michezo na siasa, kwamba mpira wa miguu, hasa klabu kongwe kama Yanga na Simba, haukuwa burudani tu bali pia nyenzo ya mshikamo wa kijamii na kisiasa.
Mwaka 1974 Afrika ilikuwa bado inasaka uhuru kamili: Msumbiji na Angola walikuwa karibu kuondoa minyororo ya Wareno, Zimbabwe bado chini ya Ian Smith, na Afrika Kusini ikiwa imekumbwa na giza la ubaguzi wa rangi. Hivyo mchango wa shilingi 10,000 haukuwa fedha tu, bali ulikuwa alama ya mshikamano na mshikamano wa Afrika.
#C & P, KUTOKA KWA BWANA MICHUZI ISSA,NGULI.View attachment 3446078
Miaka ya 74, kiasi cha shs 5000/- ulikuwa unanunua nyumba mnazi mmoja,lumumba st.Kuna jambo la kufikiria hapo nimepata japo ni nje ya mada...
Ina maana miaka kadhaa mbele ukimwambia mtoto wako kua enzi zetu tulikua tunahangaika kutafuta milioni Moja anaweza akakucheka.. kama ambavyo Kwa Sasa nacheka Mimi kuskia yanga kama taasisi ilichangia elfu 10 miaka ya nyuma??
Dah Kwa hiyo itafika kipindi milioni Moja itakua ni pesa ya kununulia vitafunwa asubuhi??... Kweli maisha ni fumboMiaka ya 74, kiasi cha shs 5000/- ulikuwa unanunua nyumba mnazi mmoja,lumumba st.
Ukisikia shughuri za kijamii si vyama vya aina yoyote vyenye muelekeo wa kundi maalumu lisilohusu baadhi ya watu, mfano makanisa, misikiti, ngoma na lolote lenye kiingilio kujiunga.Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans, Mzee Mangara Tabu Mangara, (mwenye kofia), alikabidhi hundi ya shilingi 10,000 kwa Mzee Omari Londo, Mwenyekiti wa TANU wa mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1974.