Ni jambo gani linakukera kwenye Redio za Tanzania?

Ni jambo gani linakukera kwenye Redio za Tanzania?

Muda mwingine huwa naielewa serikali inapohitaji lazima wawe na degree,japo kuwa na degree Si hoja ya kuwa na uwezo wa kujenga hoja,ila itapunguza watangazaji wa hivyo wanaookotwa mitaani
 
Lugha ni tatizo kubwa watangazaji hawanolewi kabla ya kusogea kwenye microphone kama ilivyokuwa kwa RTD enzi zake kiswahili fasaha.

Uko wapi Dada Christine Chakunegela? Huenda ndiwe pekee uliyebakia na kiswahili fasaha kwa sasa.
Huyo dada sijui mama mbona bado yupo TBC na ninamsikilizaga sana tu
 
BBC swahili ilikuwa zamani. Unapata habari za kimataifa mpaka unafurahi. Siku hizi asubuhi baada ya taarifa za michezo wanaingia kwenye kujadili mada, nachukia sana, mada wanazojadili ni za ovyo ovyo hazina mashiko.
Kweli kabisa, Bbc wamepoteza mvuto walipohamia dar na nairobi hata watangazaji wao wamekuwa wa hovyo hovyo tu tofauti na walivyokuwa london.
Mimi sasa hivi nasikiliza DW tu, bbc imeshapoteza mvuto
 
Clouds FM mnazingua sana kwa jinsi mnavyoi promo hiyo show ya fiesta mnakera sana tangazo kila baada ya dakika nne.
Unajua maana ya neno Kuzingua? katka maelezo yako sijaona walivyokuzingua.
 
Mimi naanza na hawa Clouds Media Group

Clouds FM mnazingua sana kwa jinsi mnavyoi promo hiyo show ya fiesta mnakera sana tangazo kila baada ya dakika nne.

Hakuna cha maana mnazungumza ni fiesta tu. Yaani radio yenu haina maana yoyote ni issues za fiesta muda wote. Mnaboa sana.

Njia pekee ya kuvutia watu kwenye tamasha sio kuharibu vipindi vyenu ni kuwork smart tu. na watangazaji walivyo wavivu nao kila dakika wanazungumzia hiyo show as if ni sherehe ya kitaifa.

Lazima mtambue kuwa sio wote wanaosikiliza hiyo radio wanayo access ya kufika kwenye hilo tamasha hasa sisi wa mikoani.

Mfano mimi huku rombo hilo tangazo la fiesta na hayo maelezo ya fiesta ni non sense hayana faida yoyote kwangu zaidi ni kero tu. Mimi ninachokihitaji ni taarifa. nahitaji information.

Pili:

View attachment 1280875

Radio one (IPP MEDIA) na studio yao ina muonekano wa ovyo sana. studio haina mvuto kabisa. Bi Joyce kama mkuu wa superbrand mnapaswa kuboresha hii studio iwe na muonekano wa kisasa ili muweze kustream online kisasa.

Atleast iwe kama ya Wasafi Katika Radio zenye on air studio kali Tanzania, probably wasafi fm ni namba moja Tanzania.

What future hold for radio?
Modern society is image-obsessed, so radio can maintain its individuality by not following suit.

From the very beginning, the advantage of radio has been its ability to boost the imagination via the content being broadcast.

Adding images to its content could make it lose its charm and scar the future identity of radio itself.
Clouds, MATANGAZO, MATANGAZO, MATANGAZO ni tatizo sana. Kuna vipindi viwili "vilikuwa" maarufu sana siku za nyuma, Power Breakfast na Jahazi. Wameviua na matangazo ukifungua radio hii muda wowote lazima ukutane na tangazo, vipindi hivi vimekuwa kama mbao za matangazo.Hatukatai matangazo ndio uhai wa chombo cha habari lakini wanatakiwa waweke matangazo machache ya maana na rate ziwe juu sana, waachane na matangazo ya buku mbili mbili hadi mgahawa wa biriyani buguruni au mtu ana birthday wanatangaza!!!!!.
 
Unajua maana ya neno Kuzingua? katka maelezo yako sijaona walivyokuzingua.

Ili uweze kuelewa lazima uwe msikilizaji wa radio at least 14 hours a day. hayo maelezo ni 1/10 ya kinachoendelea katika media. ukiwa msikilizaji wa radio ndo utagundua hawana content.
 
Hawa watangazaji wa Entertainments , wana kastyle kao kakufanana fanana kila ufunguapo stations mbalimbali mchana utakasikia, i guess kuna Role model wao wanajaribu kumuiga, utasikia "umeona banaaa" "hapa mjengoni", "Ewh ivooo yaaaniiii".
 
Watangazaji wengi wanachukua chukua tu taarifa kutoka kwenye mitandao ya kijamii na kuzitangaza. Nyingi zikiwa ata hazina vyanzo vya kueleweka.

Kuna hii nyingine unakuta watangazaji wako zaidi ya wawili studio wanaendesha kipindi basi ova genge la wahuni ni makelele kila mtu kujiona mjuaji wanabishana wenyewe kwa wenyewe yaani ova hawapo ON AIR.

Na sababu nyingine nyingi ndio zinazochangiaga nisisikilize sana radio.
Naunga mkono maoni yako mkuu nadhani Magic fm wamekuelewa vizuri.
 
I love music na radio yenye unafuu ni kiss fm. Though nao watangazaji wao wamekuwa waongeaji sana, Unajua unapokuwa unaongea sana basi uelewe kile unachoongelea kwa facts siyo mastory ya kijiweni unayaleta kwa radio! Mimi nikiwa kwa public transport kwa safari ndefu huwa sikosi novel au headphone kwa Sababu sipendi kusikia maujinga!
 
baada ya tangazo fulani la bidhaa kuisha utasikia mtangazaji anasema "hata me natumia hayo maji yakoo bariiida sana"
"unasikia bwana kitenge hizo karanga ninatafuna sana kabla sijaja hapa kipindini"

"kifurushi hicho ni bomba saana yaani hata ile laini ya mtandao mwngne nishaiacha ..ninkuperuzi tu"

NB NDUGU HAWA WATU NI WANABOA KILA TANGAZO UNAKUTA YEYE TU ANATUMIA ila sijawahi sikia baada ya tangazo la condom kuwa kuna mtangazaji huwa anaongea lolote
[emoji16] [emoji16]
 
Kweli kabisa, Bbc wamepoteza mvuto walipohamia dar na nairobi hata watangazaji wao wamekuwa wa hovyo hovyo tu tofauti na walivyokuwa london.
Mimi sasa hivi nasikiliza DW tu, bbc imeshapoteza mvuto
Hawa bbc sijui wamepatwa na nini. Naona kila kukicha wanazoa watangazaji lukuki kutoka hizi radio za burudani/radio za fm.

Nadhan shida inaanzia hapo. bbc ya sasa sio ile tuliyoizoea kabisa. Hakuna substance.
 
Watangazaji kuongea ongea kiingereza wakati hata kiingereza chenyewe hawajui. Utasikia as if kama, mara still bado yaani hovyo kabisa
kuna mambo yanakera sana. Kuna wakati nilijikuta nasikiliza kipindi cha michezo cha kiingereza cha tbc, kilikuwa kinarushwa jioni/usiku.

kilikuwa na watangazaji wawili wa kiume wakiongea kiingereza. Ilikuwa ni dhahiri watangazaji hawa hawajui lugha hii.

Sijawahi kusikia kiingereza kibovu km kilichokuwa kinatumiwa na hawa watangazaji wa radio ninayoamini ilipaswa kuwa kioo kwa radio zingine hapa nchini.

Wakati mwingine unajiuliza "hawa si waongee kiswahili tu" maana wanachoongea sio kiingereza bali walikuwa wanatafsiri kiswahili kwenda kiingereza tu.

Inatia shaka sana kama haya yanaweza kutokea kwenye radio kongwe yenye hazina ya uzoefu na utalaam wa mambo ya habari.
 
Kuna tangaxo la kijinga la kondomu zakije lile neno kujamiana sijui waliliweka lann Yan wajinga Sana Kaz ya kondom inajulikana

Bora usikilize DMX ubran heat
Wengine hatujuhi kazi ya ndomu
 
Japo jamaa wana uwezo mdogo wa kutangaza michezo ila nakipenda sana kipindi chao, hasa jtatu. Wengi nimeona wanakisikiliza. Waongeze tu kutafuta habari.
Hivi radio ni nani hasa? Nipe dondoo,Highlands fm,bomba fm zinamilikiwa na nani hivi brother? Bomba mtambo uko vizuri sana sema vipindi bado.
 
Back
Top Bottom