Ni jambo gani unahisi ukimwambia mwenza wako anaweza asikuelewe unabaki unavumilia tu kimya kimya?

Ni jambo gani unahisi ukimwambia mwenza wako anaweza asikuelewe unabaki unavumilia tu kimya kimya?

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Wakuu, mara nyingi tunaongelea suala la kuwa na uwazi lakini pengine bado mahusiano mengi wanaishia migogoro kwasababu wanashindwa kuendana na maana kuu ya huo uwazi.

Unakuta kuna mtu hawezi kumwambia mwenzake labda ananuka kwapa, au ananuka mdomo, anabaki anavumilia tu kimya kimya akiamini kwamba akimfungukia atakasirika.

Mimi kwa fikra zangu naona uwazi una uwanda mpana sana katika mahusiano. Yaani hata details ndogo ndogo unazoona mwenza wako atakasirika inatakiwa umwambie tu, atakasirika sawa lakini ukweli ndo ushampa.

Wewe ni jambo gani kila siku unashindwa kumwambia mwenza wako unabaki unamvumilia tu?
 
Back
Top Bottom