Sio kwa kujisifia lakini kama unamiliki chombo cha moto na unaweza kumfundisha mtoto, sioni kama kuna cha kukuzuia.
Elimu sio darasani tu, kumfundisha mtoto kitu chohote kinachoweza kuwa na faida ni elimu.
Mwaka una wiki 52 na siku 365.
Je, umeshindwa kutenga muda kwa mtoto wako, hasa wa kiume, ili kumfundisha kuendesha gari au pikipiki?
Mtoto anafika miaka 14 na hajui kuendesha hiyo ni aibu kama ulikuwa na uwezo wa kufundisha
Mimi nina mtoto wa darasa la tatu, lakini tangu mwaka jana akiwa darasa la pili, nilianza kumpakata na kumfundisha kunyoosha steering wheel (msteringi), na hadi mwaka unaisha, alikuwa ameiva.
kipindi hiki, hata tukiingia barabara zisizo na magari mengi anayoosha kwa ustadi, anajua kazi ya indicator, upande wa kuendeshea uwe kushoto, na anajua pia kunyoosha reverse tukiwa tunatoka nyumbani.
Mwaka ujao taratibu ataanza kujifunza kuendesha bila kupakatwa
Miaka 18 aende driving school hata ya wiki mbili, apate leseni yake ya kuweze kuingia rasmi barabarani.
Kwa miaka 14 bado haruhusiwi kuendesha gari barabarani, lakini usimwache kuwa mgeni wala kuwa na hofu ya kutojua kuendesha. Kufundishwa mapema kuna umuhimu mkubwa, kwani atakuwa tayari na ujuzi wa kuendesha kabla ya wakati.