Ni jambo la hatari sana kutoa ushuhuda wa uongo!

Ni jambo la hatari sana kutoa ushuhuda wa uongo!

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
5,718
Reaction score
7,784
Hali hii naona ifike mahali itazamwe kwa jicho la tatu. Ukiwatazama hawa wanaojiita Mitume hasa kwa hapa DSM, kwa kweli kuna utata mno kwao, na kwenye baadhi ya shuhuda za wafuasi wao.

Kwa akili ya kawaida tu ni wazi kuna watu wafuasi wanatoa shuhuda za uongo na sijajua ni kwa maslahi ya nani.

Kama raia huru kikatiba, nina haki ya kuhoji na kuwa na wasiwasi pale ninapoona baadhi ya mambo kwenye nchi yangu si ya kawaida.

Kuna haja ya hawa wafuasi wanaotoa hizi shuhuda kuanza kufuatiliwa kwa makini, ili kuhakikisha ni kweli au ni uongo, ukizingatia kwamba shuhuda nyingi ni kama 'vituko' kwa kweli.
 
Hata ukijua ni uongo itakusaidia Nini?
Mkuu mambo ya rohoni ni magumu kuyapima kwa macho. Hiyo ni bahari unayo taka kuivuka kwa kupiga mbizi, hutaweza. Abudu kivyako, focus kwenye mambo yako, maisha yako na Mungu wako!!!
 
Back
Top Bottom