Ni jambo la kutisha mno kufikiria kwamba Kuna siku ccm itaondoka madarakani kwa sanduku la kura ! Kitakacho iondoa ccm madarakani ni kiyama tu !

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Kabla sijatoa sababu za kwanini ni ngumu sana kuiondoa ccm madarakani nitaorodhesha majina ya wababe waliowahi kujaribu kuiondoa ccm madarakani na Hali zao kwa sasa ,1995 ndio Kila mtu aliamini kazi imekwisha ,wanasiasa nguli walijiondoa ccm na kuunda ngome imara Sana ya ushindani na Kila mtu aliamini ccm imeondoka ,Augustine mrema,makongoro Nyerere ,mabele marando ,Christopher mtikila ,mzee mtei ,sengondo mvungi ,na makachero kadhaa kutoka ccm waliibomoa kabisa ccm Kila mahali lakini mwisho waliangukia pua ,2000-2005...freeman mbowe..chacha wangwe .Christopher mtikila ..dk wilbroad slaa ! Zitto kabwe ..jemsi mbatia,mabere marando ,Augustine mrema ,samson mwigamba...na wengine wengi Bado waliangukia pua japo 2005 ushindani haukuwa mkubwa sana...2015 --2020 Edward lowassa ,Bernard membe ,zitto kabwe ,freeman mbowe ,na vichwa vingi kibao lakini Bado waliangukia pua ...hivyo ndio vilikuwa vizazi chuma ,miamba kweli kweli ,watu wabishi ,wakiamua lao liwe linakuwa ,Hawa jamaa walikuwa wakiamua ni maandamano hakuna wakuwazuia ,najiuliza kizazi hiki Cha akina mnyika kitaweza kuiondoa ccm madarakani kwa sanduku la kura ? Tuimalishe vyama kwa ajili ya kukidhi matakwa ya kidemokrasia lakini tuachane na mawazo ya kuiondoa ccm madarakani haitawezekana kwa kizazi hiki Cha watu waoga kupitiliza na vijana wa hovyo kuwahi kutokea !!
 
Kinachoiweka CCM madarakani ni kuwa Chama Dola, maana yake vyombo vyote vya Dola yakiwepo Majeshi yote, Mhakama, Tume ya Uchaguzi na Katiba inayompa Mdaraka ya Mungu mtu Rais ambaye ndiye mwenyekiti wa CCM. Tunashuhudia jinsi wapinzani wanavyotekwa, kuteswa na kuuwawa na vyombo vya dola kama mbinu moja wapo ya kuudhoofisha upinzani na kuinufaisha CCM.

Kwa vile CCM inatawala kwa mkono wa chuma wa vyomvo vya dola basi ni vyombo hivyo hivyo vitakavyoiondoa CCM madarakani. Si watumishi wote wa vyombo hivyo vya dola ambao wanafurahishwa na kuridhika na jinsi wanavyotumika kuiweka CCM madarakani bali ni viongozi na makamanda wao wanaonufaika na mfumo huu ambao kwa idadi ni wachache sana ukilinganisha na hao wanatumikishwa. Itafika wakati hawa askari na watumishi wa ngazi za chini wa vyombo hivi watachoka udikteta na wataamua kuasi amri haramu za makamanda wao wanaokula na watawala na huo ndiyo utakuwa mwisho wa CCM. Itachukua muda lakini kwa hakika kabisa wakati huo utafika hivyo nakataa kuwa CCM itatawala milele yote.
 
Kabla sijatoa sababu za kwanini ni ngumu sana kuiondoa ccm madarakani nitaorodhesha majina ya wababe waliowahi kujaribu kuiondoa ccm madarakani na Hali zao kwa sasa ,1995 ndio Kila mtu aliamini kazi imekwisha ,wanasiasa nguli walijiondoa ccm na kuunda ngome imara Sana ya ushindani na Kila mtu aliamini ccm imeondoka ,Augustine mrema,makongoro Nyerere ,mabele marando ,Christopher mtikila ,mzee mtei ,sengondo mvungi ,na makachero kadhaa kutoka ccm waliibomoa kabisa ccm Kila mahali lakini mwisho waliangukia pua ,2000-2005...freeman mbowe..chacha wangwe .Christopher mtikila ..dk wilbroad slaa ! Zitto kabwe ..jemsi mbatia,mabere marando ,Augustine mrema ,samson mwigamba...na wengine wengi Bado waliangukia pua japo 2005 ushindani haukuwa mkubwa sana...2015 --2020 Edward lowassa ,Bernard membe ,zitto kabwe ,freeman mbowe ,na vichwa vingi kibao lakini Bado waliangukia pua ...hivyo ndio vilikuwa vizazi chuma ,miamba kweli kweli ,watu wabishi ,wakiamua lao liwe linakuwa ,Hawa jamaa walikuwa wakiamua ni maandamano hakuna wakuwazuia ,najiuliza kizazi hiki Cha akina mnyika kitaweza kuiondoa ccm madarakani kwa sanduku la kura ? Tuimalishe vyama kwa ajili ya kukidhi matakwa ya kidemokrasia lakini tuachane na mawazo ya kuiondoa ccm madarakani haitawezekana kwa kizazi hiki Cha watu waoga kupitiliza na vijana wa hovyo kuwahi kutokea !!
Kwanza wewe umejiandikisha kupiga kura ? tuanzie hapo kwanza.

CCM ukuwauliza idadi ya wanachama wao waliojiandikisha kupiga kura wanaweza kukutajia. Je matawi/ kanda za CHadema wanajua wanachama wao wangapi wanejiandikisha hadi sasa? Nimeulizia chadema kwa sababu nchi hii vyama ni viwili tu.

Wafu wako radhi waingie uwanjani saa saba jua kali wasubirie mechi saa kumi na nusu lakini hawako tayari wapange foleni kwa nusu saa tu ili kujiandikisha. Kupoga kura.

Kelele tunazosikia sasa tika chadema ni maandalizi ya kisaikolojia watakaposhindwa uchaguzi ionekane uchaguzi haukuwa wa haki.

Kama jweli chadema ingekuwa ina wanachama milioni 15 au hata milioni saba halafu hao wanachama wajiandikishe kupiga kura, je wasingeshinda kwa kishindo sehemu nyingi hata kama kuna watoto wameandikishwa?
 
Back
Top Bottom