Ni jiko gani lina gharama zaidi kwenye matumizi kati ya la gesi na la mkaa?

Ni jiko gani lina gharama zaidi kwenye matumizi kati ya la gesi na la mkaa?

deejaywillzz

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2014
Posts
637
Reaction score
224
Habari wakuu.

Nataka nifanye ubunifu wa kutengeneza majiko ya plate na kukaangia chips ambayo yanabana matumizi. Lakini kabla ya hayo nataka nijue kati ya Gesi na Mkaa katika matumizi ni ipi inabana matumizi.
 
Jiko la mkaa ni gharama nafuu ukilinganisha na gesi,gunia la elfu 40 unaweza kupikia hata mwezi mzima lakini gesi thubutu.
 
Mkuu inategemea na jinsi maisha uayoishi. Kwangu gesi 15 kg natumia siku 40. Ikipikwa mboga ya Taifa nanunua mkaa wa buku. Gesi bei ni elfu 50 mitaa yetu. Maisha yana kwenda. Tengeneza jiko nafuu la gesi sio mkaa. Mkaa unaharibu mzingira.
 
Gesi ni nafuu zaidi kwani lina save muda,lakini pia bei ya gesi na mkaa havitofautiani sana
 
Habari wakuu, nataka nifanye ubunifu wa kutengeneza majiko ya plate na kukaangia chips ambayo yanabana matumizi. Lakini kabla ya hayo nataka nijue kati ya Gesi na Mkaa katika matumizi ni ipi inabana matumizi.

Kwa nyumbani gas ni nafuu lkn pia hata kwa biashara inaweza kuwa nafuu maana naona watu wengi wakitumia gas siku hizi, zaidi kwa hapa dar. Maana kuna maeneo mengine mkaa wanapata kwa bei nafuu.
 
Unafuu inategemea na mahali ulipo, kuna maeneo mkaa gunia ni sh 10,000/= lakini maeneo mengine zaidi ya 40,000/= sasa lazima ufanye consideration ya eneo kabla ya kutoa jibu
 
Gas iko poa...sio gharama kiivyo pia iko fasta
 
inategemea na matumiz mi ges natumia miez mnne kasoro nipo pekeangu na napka sana had maji ya kuoga huchemsha.
sijajua mkaa nikiwa pekeangu.
ila ges expres differ na mkaa
 
Ukitaka kuenjoy kuwa na vyote gas na mkaa mfano,
mim natumia gas ya kg15 kwa miez5 hasa kwnye chai,mazwa na uji wa mtoto,kupasha chakula na maji ya kuoga

mkaa nautumia kwnye vitu vigumu kama maraga,makande,wali,nyama etc

so unakta kwa huk kijijn mkaa wa 7,000/= unakaa mwez mzima na gas inaweza kusarvive kwa 5months,

karibuni sana kigoma,
 
Unafuu inategemea na mahali ulipo, kuna maeneo mkaa gunia ni sh 10,000/= lakini maeneo mengine zaidi ya 40,000/= sasa lazima ufanye consideration ya eneo kabla ya kutoa jibu

Gunia la Mkaa Dar lile la Lumbesa ni elfu 70
 
inategemea na matumiz mi ges natumia miez mnne kasoro nipo pekeangu na napka sana had maji ya kuoga huchemsha.
sijajua mkaa nikiwa pekeangu.
ila ges expres differ na mkaa

Mmh best miezi minne? Kg ngap huo mtungi? Labda kama unaishi mwenyewe na sio mtumiaji wa mara kwa mara, nijuavyo mie gas huisha baada ya mwezi kwa matumiz ya familia, kama bachelor ata miwil au mmoja na nusu, ila miezi minne mmh
 
Gunia la Mkaa Dar lile la Lumbesa ni elfu 70

Gas mtungi sh 50 elfu mpaka 60, gas is the best, haichafui nyumba na ni cheap, mambo ya mkaa labda akiba tu kwa ajili ya maharage na vitu vigumu
 
Ukitaka kuenjoy kuwa na vyote gas na mkaa mfano,
mim natumia gas ya kg15 kwa miez5 hasa kwnye chai,mazwa na uji wa mtoto,kupasha chakula na maji ya kuoga

mkaa nautumia kwnye vitu vigumu kama maraga,makande,wali,nyama etc

so unakta kwa huk kijijn mkaa wa 7,000/= unakaa mwez mzima na gas inaweza kusarvive kwa 5months,

karibuni sana kigoma,

Weee...!
Miezi mitano? Hongera
 
Maharage, nyama natumia pressure cooker so gas inahusika.
Mkaa napikia kande, ndizi za kuunga nazi ( naona tu zinanoga kwa mkaa)

Gas 15kg natumia zaidi ya mwezi ila haifiki miwili, mkaa Gunia linakaa hadi nasahau.
 
Gesi ni nafuu zaidi kwani lina save muda,lakini pia bei ya gesi na mkaa havitofautiani sana

yes nilikaa nikafikiria kuwa unanunua mkaa buku kila siku mwisho wa siku unajikuta matumiz ya mkaa yapo juu Mara siku ukute mkaa umeisha ni shidaa..lakini gesi linasave time,clean energy..15kg mimi natumia 2month na ushee.hata bei havitofautian sana na gunia la mkaa..kwa mini usivute gesi mkuu
 
Gas mtungi sh 50 elfu mpaka 60, gas is the best, haichafui nyumba na ni cheap, mambo ya mkaa labda akiba tu kwa ajili ya maharage na vitu vigumu

  • Mkuu inategemea na jinsi maisha uayoishi. Kwangu gesi 15 kg natumia siku 40. Ikipikwa mboga ya Taifa nanunua mkaa wa buku. Gesi bei ni elfu 50 mitaa yetu. Maisha yana kwenda. Tengeneza jiko nafuu la gesi sio mkaa. Mkaa unaharibu mzingira.​

Jamani bei ya 15kg ni Tshs 45,000/= hapa DSM. Pia mimi natumia mkaa na gesi kwa matumizi tofauti naona vikiwa pamoja kuna unafuu mkubwa sana. Chai, uji wa mtoto, maji yakuoga ukiwasha mkaa inakula kwako kwani unatumia chinin ya asiliamia 50 ya nishati inayozalishwa lkn gesi unatumia 100% na hivyo kusave. Ukipika mboga ya shule ama makande kwenye gesi inakula kwako.

Kuna mtu kaongelea usalama, kwa kweli gesi ya sasa ni tofauti na zamani kwani kuna jerry (panya) alikula lile pipe la kupeleleka gesi kwenye jiko nikasikia harufu kali na kutafuta chanzo na kurekebisha ingekuwa ile ya zamani nafikiri tungeongea mengine sasa kwani ilichukua muda kugundua.
 
Back
Top Bottom