Pre GE2025 Ni Job Ndugai pekee anaeweza kuishake CCM uchaguzi ujao! Muhimu ni wapinzani kuungana wamshawishi awe mgombea kupitia CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hawataki ushauri
 
Ninavyomfahamu Job hawezi kuhama CCM kwa tamaa tu ya u-Rais; vivyo hivyo CDM chini TAL hawawezi kurudia makosa ya 2020 walivyomuachia EL kugombea. Hebu wajisimamie wenyewe waingie ulingoni wasitegemee wahamiaji..!
Hawataambulia hata kiti kimoja
 
Watanzania wa mkoa gani ? Tena na hivi anajifanya mjuaji ndio hatumpi hata kura moja
Yule hajifanyi mjuaji, bali anajua. Ila kilaza kama wewe ndiye unaishia kukereketwa
 
Umeandika ujinga tupu
 
Kupigwa hakumfanyi awe na uwezo wa kuongoza nchi
Historia ya dunia haijawahi kuwa na shujaa wa kupewa mezani kama Samia .
Ndio maana ama nchi itawaliwe kijeshi au na mpigania haki na mpinga dhulma na ufisadi ndio inapata maendeleo .
 
Hilo sio jambo la kujivunia ni ujinga
Mbona mnajivunia Wa asira na Samia ambaye hajawahi kugombea wala kuomba ridhaa ya kugombea na kuchuana na wenzake ili tuone nini maono yake na mipango yake na namna atakavyolinda rasilimali za nchi .

Maana mpaka sasa tuna rais ambaye hana mpango wa kulinda Rasilimali za nchi . Hii si hatari kubwa sana . Yaani hana mpango kabisa wa kulinda Rasilimali za Watanganyika kwa namna yoyote katika Ulimwengu uliojaa vurugu za kugombania rasilimali za asili.

Hapa tunawezaje kusema tuna mgombea urais wa nchi au ni dalali wa nchi . Kumchagua mtu ambaye anakaa na kuwaza kuuza rasilimali za nchi kinyume na sheria ni tatizo kubwa sana. Urithi pekee wa dunia huu ni rasilimali za asili na namna ya kuzitumia kwa manufaa ya wenyeji.

Waarabu tunakoenda mafuta yatapata ushindani kwenye nishati kutokana na teknolojia ya kisasa ya nishati isiyotumia mafuta .

Cha ajabu tumepata Rais anayewapa tena waarabu kile kitu ili tena wageuze rasilimali zetu kuwa zao na kunufaika nazo na sisi kuwa wa kusubiri misaada ya kujengewa nyuma za ibada na visima vya maji na kuwa vibarua wao .

Wakati wa Afrika kuamka na kuwafukuza marais wote wanaochezea Rasilimali za nchi ni huu.
 
Ndugai hawezi fanya ujinga huo kamwe!
Ndugai hata ubunge uchaguzi ukiwa huru hapati. Hivi mnadhani mtu aliye chama cha upinzani na ana wafuasi wengi ni wa mchezo? Huko hakuna kubebwa na dola na kusombewa mashabiki kama CCM. Samia leo akisimama bila kofia ya urais hapati hawa watu kumi. Uliona Membe (RIP) alipotoka CCM alihutubia viti na meza wakati huko CCM aliingia kwenye listi ya wagombea wa urais wenye ushawishi?
 

Usilolijua ni usiku wa kiza.

Unafahamu kilichomfanya aachie ngazi ya uspika?
 
Upinzani una watu wanao jitosheleza ,mapandikizi hakuna, Ndugai ana lipi? Hana jipya.

Mpaka sasa ccm haina mgombea ambaye anaweza kuja upinzani na kushutu nyoyo za watu , hata SSH leo akatokea akaja upinzani hauziki
 
Mwenda wazimi Ngugai hata jimboni kwake hawezi kushinda mpaka abebwe na polisi, ndio unaona anafaa kugombea kupitia upizani. Sio bure na wewe utakuwa mgojwa wa akili kama ndugai.
 
Unamaanisha kuwa CHADEMA wameishiwa wagombea kiasi hicho mpaka wakakope Maccm mgombea? Tena mzee wa Kapernaumu?
Chadema sio kama ccm wanaowapa wagonjwa kama Wassira kuwaongoza!! Ndugai is a sick man akae huko huko ccm na Samia!
 
Sema wanasiasa wana tamaa sana,hivi kama umepewa ulinzi na unalambishwa asali 80% ya anayolamba aliyeko madarakani,kuna haja gani ya kuanza kukimbizana na mdaraka!! Mfano Spika wa Sasa analamba 30M,yeye atakuwa analamba 24M ,je hazitoshi hizo?
Wana tamaa sana halafu wenzao wanawaambia wajiajiari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…