Ni kada gani unastaafu ukiwa na cheo Cha juu kiinua mgongo mil 80-100?

Ni kada gani unastaafu ukiwa na cheo Cha juu kiinua mgongo mil 80-100?

Kama wewe ni mtumishi wa umma hakikisha yafuatayo unayafanya kabla hujafikisha miaka 45.

1. Hakikisha una mashamba karibu na mahali unapopanga kustaafu.
2. Hakikisha watoto wako wanapata malezi bora na elimu bora, utavyostaafu wasije geuka tegemezi kwako.
3. Hakikisha umenunua viwanja vya bei rahisi nje ya mji, miaka 20 baadae hakutokuwa nje ya mji tena, ukijenga appartment basi utakuwa unapokea kodi maisha yanaenda. Mfano leo Kimbiji na Chanika vipo viwanja hadi vya 2mil, wewe nunua huko, tena unalipia kidogo kidogo. Fanya ujenzi wako taratibu hata kwa miaka 10, ukishastaafu hizo nyumba zitakufaa.
4. Tengeneza mazingira ya kukopesheka benki kibiashara, fanya low risk business, by the time unastaafu utakuta unakopesheka 1bil wakati pension yako ni 100mil.
 
Tupe stry ilikuaje????
Mjomba wangu alipata Tsh 70 Million, aakacha kwanza mke. Akaja Dar akanunua Nissan Hard body used kwa Tsh 20 Million

Then Tsh 40 Million akaweka kwa microfinance moja ilikuwa pale Masaki inaitwa Bestway Capital Management.

Mwaka 2021 wakati wa COVID-19 walilizwa vibaya

Screenshot_20250605_170731_Chrome.jpg
 
Ni zaidi ya milioni 100, ungesema kuanzia 150 M+

1.Uhasibu ukiwa na CPA hasa kama ulikuwa unafanyia taasisi za kodi na fedha za serikali (TRA, NSSF, BOT, n.k.)

2. Civil Engineering, Mechanical Engineering na Electical Engineering kwenye taasisi kama Tanroads, Temesa, TBA, n.k.

3. Wildlife conservation - TANAPA

4. Sheria - mahakimu wa serikali

5. Lecturers wa vyuo vya serikali

6. Idara za ulinzi hasa Jw na Polisi - ukiwa na elimu kubwa ndani ya jeshi

7. Madaktari bingwa - Muhimbili na hospitali za rufaa

8. Maafis ugavi wanaohusika kununua mahitaji ya serikali na kutoa tenda
Namba 8 si sawa. Hao hujilipa wenyewe kabla ya kustaafu kwani kamba zao ni ndefu sana.
 
Ata ukipata hicho kiinua mgongo wakati mwili ulishachoka haikusaidii zaidi ya kuitumia katika kuuripea huo mwili tu.
Fanya kinachowezekana mapema kwa kukopa n.k
 
Back
Top Bottom