Ni kama vile Vunjabei anaelekea kufilisika

Vipi unahisi ka faraja flani ee
 
Unapata wapi huo mda wa kufutilia biashara ya mtu kiasi hicho?huo mda ungeuza hata barafu ungesogea kidogo kwenye maisha yako
Unapata wapi kufuatilia mada ya mtu, si uanzishe ya kwako. Unapata wapi muda wa kutumia JF ya Maxence Melo, si uanzishe yako utype mkono wa kulia na ujijibu mkono wa kushoto.

Si twende hivyo eti?
 
Kwa hizo picha ni wazi kuwa hujui duka la vunjo bei lilipo hapa Iringa
 
Majungu ndo kazi pekee wakosa kazi huifanya kwa uaminifu mkubwa
 
So kazi yako ni kuzunguka nchi nzima kufanya tathmini ya biashara zake? Fine,muongezee mtaji ama uache kufuatilia yasiyokuhusu
 
Pambana sasa na wewe uchomoze,,,Kupanda na kushuka ni Jambo la kawaida kwenye upambanaji hakuna alie Bora,,,hakuna alie dhaifu,,,Tupo kwenye mhimili wa Maisha,,Acha Roho mbaya ya kimaskini.
Hii nchi kumbe ndio maana ina machawa tu, tunaweza kuwa tunalaumu viongozi ila wanaowazunguka ndio sampuli hizi zenu humu. Jamaa kauliza swali kama Vunjabei anaelekea kufirisika, kwa wenye akili ambao hawajazaliwa na wachawi na waganga wa kienyeji hilo ni swali la kawaida halina wivu au roho mbaya.

Ni suala la kujadili kibiashara, kwamba Vubjabei kawekeza kwenye madawa ya binadamu nguo anaona zimevamiwa, kapata sekta nyingine inayomlipa zaidi, au kapata ushindani, au ameuza brand, au aliingia kwenye nguo akiwa na exit plan na mpango wake umetimia. Sasa badala mjadili kibiashara sababu yeye mwenyewe aliileta public biashara yake hivyo ni lazima ijadiliwe. Nyinyi mnaijibu kama waganga wa jadi, wachawi, wenye wivu, wanafiki.

Kwani biashara inatakiwa izungumziwe kwa sifa tu, hakuna kuhoji au kuuliza?
 
Mpwaa umeamua kumkagua kabisaaa tupe na mikoa minginee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…