Ni kanda ya Magharibi pekee haijawahi kuwa na kiongozi wa kitaifa - wanasiasa mna majibu? Nielimisheni!

Ni kanda ya Magharibi pekee haijawahi kuwa na kiongozi wa kitaifa - wanasiasa mna majibu? Nielimisheni!

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2020
Posts
1,809
Reaction score
1,692
Wabobezi wa siasa, nijengeeni uwezo!

Kanda ya Magharibi - yenye mikoa ya Kigoma na Tabora ndiyo haijawahi kuwa na kiongozi wa kitaifa - nalenga Rais au Makamu wa Rais au Waziri Mkuu.

(a). Orodha ya Marais tangu 1961 - 2021
= Mwl Julius K Nyerere (kanda ya ziwa); Mzee Ally Hassan Mwinyi (Zanzibar); Benjamin William Mkapa (Kusini); Jakaya Mrisho Kikwete (Mashariki); Dkt John Pombe Magufuli (Ziwa); na Samia Suluhu Hassan (Zanzibar).

(b). Makamu wa Rais
= Abeid Aman Karume (Zanzibar); Aboud Jumbe (Zanzibar); Ally Hassan Mwinyi (Zanzibar);

* Joseph Sinde Warioba (Ziwa); John Samwel Malecela (Kati); Cleopa Msuya (Kaskazini); Omary Ally Juma (Zanzibar); Ally Mohammed Shein (Zanzibar); Mohammed Gharib Bilali (Zanzibar); na Samia Suluhu Hassan (Zanzibar).

(c). Mawaziri Wakuu tangu 1961 - 2021
= Julius K Nyerere (Ziwa); Rashid Mfaume Kawawa (Mashariki); Edward Moringe Sokoine (Mashariki); Cleopa Msuya (Kaskazini); Edward Moringe Sokoine (Mashariki); Salim Ahmed Salim (Mashariki); Joseph Sinde Warioba (Ziwa); John Samwel Malecela (Kati); Cleopa Msuya (Kaskazini); Fredrik T Sumaye (Kaskazini); Edward Ngoyai Lowassa (Kaskazini); Mizengo Kayanza Peter Pinda (Nyanda za Juu Kusini); na Kasim Majaliwa Majaliwa (Kusini).

Kwa uchambuzi huo hapo juu inaonesha mikoa ya Kigoma na Tabora tangu Uhuru wa nchi yetu na baadae Muungano haijawahi kuwa na kiongozi wa kitaifa kwa nafasi za Rais, Makamu, au Waziri Mkuu. Mpo wabobezi na wachambuzi wa siasa na utawala - hebu njooni na kile mnachodhani ni chanzo cha sababu za kutokuwa na walau moja kati ya nafasi hizo.

Aidha, nimempigia saruti Hayati JPM kwani kwa uongozi wake aliliona hili ndipo akamteua Dkt Philipo I. Mpango (WF); Prof Joyce Ndalichako (WE).

Nahitimisha kwa kusema
"Hili ni taifa la watanzania kwa kuzingatia mipaka yake na kwa vyovyote vile watanzania wote tunazo sifa sawia".

Msakila M Kabende
Kakonko - Kigoma (Tanzania)

******************
Mhe Mama Samia, kigoma na kanda ya magharibi tunakupongeza kwa uteuzi huo - tunakuhakikishia ushirikino ktk chama na Serikali
 
Mbona yule Mpimbwe Mizengo ni wa kanda yenu kabisa mkuu? Manaake kwa nnavyoona Katavi iko affiliated zaid na Kigoma kuliko kuiweka kundi moja na Mbeya/Njombe/Iringa na Songwe

Halafu rekebisha Moringe alitokea Kaskazini ya wapi?
 
Umeshasoma katiba ya Tanzania, badala ya kukujibu ni heri ukasome ili ujue sifa za rais na jinsi anavyopatika pia angalia kama kuna kigezo cha kuchagua rais kutokana na kanda anayotoka.
 
Huu uzi umekosa maana kwa kutojua hata hizo Kanda zinajumjisha mikoa ipi.
Kanda ya magharibi Ina mikoa ya ; Tabora, Katavi na Kigoma
Mizengo Linda kwao ni mpimbwe, na mpimbwe ipo mkoa wa katavi
 
Huu uzi umekosa maana kwa kutojua hata hizo Kanda zinajumjisha mikoa ipi.
Kanda ya magharibi Ina mikoa ya ; Tabora, Katavi na Kigoma
Mizengo Linda kwao ni mpimbwe, na mpimbwe ipo mkoa wa katavi
Kanda ya magharibi ni mkoa wa Kigoma na Tabora bwana
 
Mtoa hoja,kumbushia kuunganishwa kwa barabara na kuimarisha viwanja vya ndege,na kuharakisha upembuzi yakinifu katika ujenzi wa treni ya mwendo kasi.
Umeme wa "grid" umefika Wilaya zote na vijiji.
Masuala ya kupata viongozi yafuate baadae,kwani hata wakichaguliwa huwa hawakai wa kuishi mikoa waliyotokea!!
 
Mbona yule Mpimbwe Mizengo ni wa kanda yenu kabisa mkuu? Manaake kwa nnavyoona Katavi iko affiliated zaid na Kigoma kuliko kuiweka kundi moja na Mbeya/Njombe/Iringa na Songwe

Halafu rekebisha Moringe alitokea Kaskazini ya wapi?
Arusha
 
Hiyo mikoa inaongoza kwa upinnzani .Upinzani wote toka Nyerere hadi vyama vingi ulianzia huko

Pinda ni mchaga?
 
Unataka tuingize mamluki wa "Kihutu" Ikulu?
 
Shida ni nini watu wote ni watanzania sio makabila au kanda
 
Kanda ya Magharibi bado mnayo kazi kubwa ya kusomesha Vijana na kuandaa ili wawe Viongozi. Vinginevyo mtabaki kuwa wasindikizaji tu hata hao uliowataja bado hawatoshi kuwa Viongozi wakuu wa Nchi.
 
Kawawa ametokea mkoa wa Lindi ni Kusini si Mashariki.

Mtoa mada nadhani analengo la kushawishi VP atokee Kanda ya Magharibi
 
Back
Top Bottom