Ni katiba mpya pekee itayoweza kuzuia ufisadi huu unaoenda kufanyika vinginevyo ni ni maumivu kwa taifa letu

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Lazima mapema iwezekanavyo tuwe na katiba mpya ambayo itaweza kumdhibiti na kumuawajibisha rais anayetumia madaraka vibaya.

Rais ambaye anaweza kugeuza ikulu ni mahala pa biashara na kutumia mwanya huo kushirikiana na wajanja wachache kujitajirisha huku wananchi wakibaki na umasikini mkubwa.

Tuwe na katiba ambayo kama bunge likishindwa kuisimamia serikali kwa uzembe wowote tunawatua wabunge majimboni kwetu.

Leo hii rais akiwa ikulu anafanya anavyotaka sababu hatuna katiba iliyowapa wananchi meno ya kumuadhibu. Hata kama atafanya masuala yasiyofaa.

Watanzania wote tunaopenda taifa letu lisiibiwe kwa manufaa ya kizazi hiki na kinachokuja tupiganie katiba mpya. Ufisadi sasa umerudi kwa kasi kubwa.
 
Ni kweli kabisa.
Bila Katiba mpya, huu ufisadi unaofanywa na watendaji wa Serikali, utaendelea Hadi mwisho wa Dunia! 🥺
 
Awamu ya 4 ilijaa majizi na tulizungumza , navyoona itapendeza tujadili ufisadi wa awamu ya 5 kwanza maana ulifichwa kwa nguvu na gharama zote.

Serikali ya awamu ya 5 ndio ilizaa ya 6 hakuna mabadiliko makubwa sana hapa.

Mwezi wa 4 ndio unaishia hivyo Majaliwa alituambia SGR inaanza majaribio vipi imeshaanza?

NB:Majaliwa ameudumu awamu zote 2
 
Wewe nawe unatosha,unajaribu kuhangaika na chuki zisizo kuwa na maana,kwenye itawala wa jiwe nani alikuwa anaiba?
 
Ufisadi ufisadi ufisadi... Bila katiba mpya, kuikata minyonyoro ya kuzivuta pesa za umma kwenda kwenye mifuko ya watendaji wengi wa serikali tukianzia na jumba jeupe ni ndoto. Watanzania tutapiga kelele sana while kakikundi cha wachache wenye mikono mirefu wakitucheka na kuendelea kunufaika kwa uwepo wa hii katiba mbovu.
Alafu anatokea kibabu flani kinasema eti katiba mpya si hitaji la watanzania kwasasa, kisa kilipewa uwakilishi wa nchi flani America huko na mwendazake...corrupted head!
 
Shida Raia wako tiyari?
 
Integrity ni Jambo Gumu Sana kwa viongozi wa Africa. Kenya walibadilisha katiba yao na ukiangalia Mambo mengi ya katiba pendekezwa ya warioba etc vitu vingi tumechukua from Kenya.Lakini angalia jinsi Kenya ufisadi ulivo mkubwa kuliko hata Tanzania.
 
Katiba haizuii uwizi kutendeka, wala haizuii umasikini, kinachozuia hayo yote ni kujielewa na kujitambua kwa viongozi, ndipo kuheshimu na kufuata kwa sheria kunakuja.

Kama katibaa ya sasa ina kila sheria zinazowabana wahuni lkn hawaogopi wala kufuata je hiyo mpya je?.

Ifike mahala tuambiane ukwel, kiongozi wa rangi nyeusi bila kuperekeshwa kibabe na kidicteta hawez fanya kazi kiusahihi..

Udicteta ndio asili ya uongozi Afrika FULL STOP
 
🤣🤣🤣🤣wacha nicheke tu. Yaani leo umekumbuka umuhimu wa katiba mpya??
 
Wewe bado hujajua umuhimu wa katiba Bora.

Nawambieni mtakuja kuitafuta wakati huo sisi hatuitaki.

Time will tell.
 
Kwa chadema wakizungumza katiba mpya wao wana agenda zao za siri za mambo machache wanayotaka.
1.Tume huru ya uchaguzi, ambayo wasimamizi wa uchaguzi watajitokeza wachaga wengiiii ili matokeo watangaze wachaga wenzao washind.
2. Kumpunguzia Rais madaraka,hili lipo kimtego, incase (haitokuja kutokea)chadema wakipata urais madaraka ya Rais yataongezwa .pumbav zao
 
katiba mpya... itapunguza mfumuko wa bei... kila mtu atakuwa na pesa hata hasiyefanya kazi atakula... katiba mpya ni muhimu sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…