Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Lazima mapema iwezekanavyo tuwe na katiba mpya ambayo itaweza kumdhibiti na kumuawajibisha rais anayetumia madaraka vibaya.
Rais ambaye anaweza kugeuza ikulu ni mahala pa biashara na kutumia mwanya huo kushirikiana na wajanja wachache kujitajirisha huku wananchi wakibaki na umasikini mkubwa.
Tuwe na katiba ambayo kama bunge likishindwa kuisimamia serikali kwa uzembe wowote tunawatua wabunge majimboni kwetu.
Leo hii rais akiwa ikulu anafanya anavyotaka sababu hatuna katiba iliyowapa wananchi meno ya kumuadhibu. Hata kama atafanya masuala yasiyofaa.
Watanzania wote tunaopenda taifa letu lisiibiwe kwa manufaa ya kizazi hiki na kinachokuja tupiganie katiba mpya. Ufisadi sasa umerudi kwa kasi kubwa.