Ni kauli gani uliwahi kuambiwa na baba, mama au mlezi wako ambayo baadae kabisa ndio ulikuja kuielewa?

Kua uyaone mwanangu.
 
Soma sana,itakuja kukuuma siku moja,watu ambao uliwaacha nyuma wanasoma halafu wanakuja kuwa mabosi wako...
 
Katika maisha yako jitahidi ujifunze kuishi maisha ya namna zote ,hii itakusaidia katika kipindi cha furaha na tabu
 
Nakumbuka Mama yangu Mlezi alikuwa ananihamsha asubuhi saa Tisa kufanya kazi za ndani na kulala saa Sita Usiku na alikuwa akiniambiaga utakiona cha mtema kuni yaan nyumba hii mpk uhame ila cha ajabu kahama yeye na Yale mateso kwangu yamenifunza jinsi ya kuishi na walimwengu like hata siku wife akivinuna napiga usafi ndani na nje ya nyumba yangu napika msosi wangu napiga na Vi serengeti vyangu viwili nalala
 
Hapana alikua mtu poa sana. Ila maneno yake tulikuja kuyaelewa baadae sana na tabu tulizipata hasa.
Katika watu wanaoona.mbali kwa watoto wao ni baba, na akiona mwenzake (mkewe) ana msikiliza atamwambia mengi kuhusu kila mtoto na maisha yake ya baadae, mama akijifanya yeye ndiye mwenye uchungu na watoto ana nyamaza anakufa nalo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…