Pre GE2025 Ni kauli ya Kishamba mno aliyotoa Chalamila, kuwa tarehe 24, majeshi yetu yote yatakuwa yanafanya usafi jijini!

Pre GE2025 Ni kauli ya Kishamba mno aliyotoa Chalamila, kuwa tarehe 24, majeshi yetu yote yatakuwa yanafanya usafi jijini!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kati ya Chalamila ambaye katoa kauli kuwa tarehe 24 ni siku ya usafi Dar es salaam na Magufuli ambaye alizuia Maandano na mikutano ya siasa kwa miaka yote ya utawala wake huku yeye akifanya kila siku nani mwovu zaidi?
Mimi naona lawama na laana zote atupiwe Magufuli muasisi wa ushenzi katika nchi iliyostaarabika
Nakumbuka jinsi alivyo wafukuza wawekezaji wa zao la korosho kwa kuwatisha na wanajeshi
 
Kati ya Chalamila ambaye katoa kauli kuwa tarehe 24 ni siku ya usafi Dar es salaam na Magufuli ambaye alizuia Maandano na mikutano ya siasa kwa miaka yote ya utawala wake huku yeye akifanya kila siku nani mwovu zaidi?
Mimi naona lawama na laana zote atupiwe Magufuli muasisi wa ushenzi katika nchi iliyostaarabika
Hi Magufuli hapa anaingiaje kwamfano? Ukiwa na stress tafuta namna bora ya kuziondoa badala ya kupigana na wafu
 
Wanajeshi wataonekana wa ajabu kama watakubaliana
 
Kati ya Chalamila ambaye katoa kauli kuwa tarehe 24 ni siku ya usafi Dar es salaam na Magufuli ambaye alizuia Maandano na mikutano ya siasa kwa miaka yote ya utawala wake huku yeye akifanya kila siku nani mwovu zaidi?
Mimi naona lawama na laana zote atupiwe Magufuli muasisi wa ushenzi katika nchi iliyostaarabika
Kwani sasa vyama vya upinzani ndiyo vina Uhuru,unaandika kama umekatwa kichwa.
Mnyika alipoenda Bungeni hakuzuiwa kutoa maoni ya chama chake? na sasa wanataka kutumia haki Yao kikatiba kuandamana wanawekewa majeshi,Samia na Magufuli ni kopo na mfuniko!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Itakuwa ni aibu kwa vikosi kutii agizo la mkuu wa mkoa.

Ipo siku ataelekea ikulu kupindua utawala kwa namna ya haya maigizo.
 
Ni nchi ya Tanzania pekee duniani ambayo Mkuu wa Mkoa anaweza kuamuru military batarian ya JWTZ iingie mitaani na mafagio eti kufanya usafi, ni fedheha kubwa.

Hili Jeshi letu litachezewa hadi lini na hawa wana siasa wetu. ? JWTZ hivi mnaona ni sawa kufanyiwa dhihaka ya kiwango hiki?
 
Ccm mmekuwa ni waoga sana kwa cdm na mnakuwa wa kwanza kukimbilia kwa wanajeshi.

Ila lazima mjue kuwa kuna siku hata hao wanajeshi watakataa huo usanii wenu
Hiyo siku ni ipi Mkuu? Maana kuna siku,kuna siku, jeshini ni UTII.

Wahuni ambao mnahamasisha watu kisha mkimbilie Canada ni wa kupuuzwa.
 
Itakuwa vizuri maana hawana kazi za kufanya hao JWTZ. Waendee wakazibue chemba za maji taka majumbani.
Sawa jichanganye siku moja utajua kuwa zipo kazi nyingi tuu, ila najua dakika 10 zitatosha kwa wewe kupangusa kamasi kwa ngumi huku unalia na kutubu.
 
Haya Sasa huyo Chalamila ndiye anapaswa kusimamia uchagizi
Huo uchagizi utakuwa salama. 🤣🤣🤣
 
Huyu mtu anatakiwa awe anaongea kati ya saa 5 - 7 akiwa 'soba' tofauti na hapo hizi kauli hazikomi
 
Nimestuka sana nilipoisikia kauli aliyotoa mkuu wetu wa mkoa wa Dar tena kanisani, kuwa tarehe 24, "anawaagiza" askari Polisi 5,000 na askari wa JWTZ 8,000 wajitokeze mitaani Dar, ili wafanye usafi!

Kustuka kwangu ni kuona Mkuu wa Mkoa, asivyoelewa majukumu ya Hawa walinxi wetu, Kwa kuwa Jeshi la Polisi nchini, wajibu wake namba moja ni kuwalinda Rais na Mali zao na JWTZ wajibu wao namna moja ni kulinda mipaka ya nchi yetu.

Nimuulize Mkuu wa Mkoa, Chalamila, hivi Kwa kuwataka hao Polisi wetu na askari wa JWTZ wafanye usafi wa Jiji, siyo kukiuka Katiba ya nchi?

Huyu aliyetoa kauli hii ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Dar na pia ameitoa kauli hiyo akiwa kanisani na ametoa kauli hiyo, baada ya kumsikia Mwenyekiti wa Chama kikuu Cha siasa nchini Cha Chadema, kutoa kauli kuwa hiyo tarehe 24 watafanya maandamano ya amani, ambayo ni haki yao kikatiba kwa kuitaka serikali kuiondoa bungeni miswada 3 ya Sheria, Kwa kuwa hiyo miswada ni kiini macho!

Huyo Chalamila ndiye anayejaribu kuivunja Katiba ya nchi waziwazi Kwa kutaka kuleta taharuki nchini, Kwa kuwa siku hiyo aliyoyaagiza majeshi ya ulinzi nchini yaingie mitaani na kufanya usafi, ndiyo siku hiyohiyo ambayo Mwenyekiti wa Chadema ametangaza kuwa wanategemea kufanya maandamano ya amani.

Najua kuwa Chalamila, ametoa kauli hiyo ili kuwatisha wafuasi wa Chadema, wanaotarajia kuandamana siku hiyo, waingie hofu ya kuandamana.

Yeye Chalamila anajua fika kuwa taarifa aliyotoa Mwenyekiti wa Chadema, ni halali kabisa, Kwa kuwa ndani ya Katiba yetu ya nchi, inaruhusu kufanyika maandamano ya amani.

Hivi tukisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, ndiye anayetaka kuleta uvunjifu wa amani ya nchi hii, nitakawa nakosea kweli?

Nimalizie Kwa kusema kuwa, kama amani ya nchi hii itapotea, basi Mkuu wa Mkoa wa Dar, awajibike Kwa kuitumbukiza nchi hii kwenye umwagaji wa damu.

Tunamwomba Mungu aendelee kuilinda nchi hii, kutokana na hao viongozi wa Chama tawala na serikali yao, kutokana na hila zao za wakati wote za kutaka kuendelea kuitawala nchi hii bila kutaka kuondoka madarakani Kwa amani
Akili ni nywele, kila mtu ana zake.

Wewe kumwelewa huyo RC katika hili, ni vigumu sana. Achana nae.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom