Ni kawaida binti wa miaka 13 kuvunja ungo?

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Habarini!

Huu ni mwaka wa 13 wa kuzaliwa binti yangu na yupo darasa la sita sasa.

Jana mama yake ananivujishia siri kuwa mtoto amekuwa (amevunja ungo).

Wadau, ni kawaida kwa binti wa miaka 13 kuvunja ungo au hii ni abnormality?!! Nilitarajia kuanzia 15 huko na kuendelea.

Uzoefu wenu tafadhali....
 
Kawaida mbona unamlisha chakula kizuri ndomana.
 

Huo ungo alikuwa kaukalia au kaweka vitu vizito hadi ukavunjika?

Jokes aside, ni kawaida na inaweza tokea kabla hata ya hapo...

Kuna mwaka nilisoma habari ya binti wa miaka 12 kupewa ujauzito, hivyo ni muda sasa wa kumlinda mwanenu...
 
Ni sawa.

Sent from my HUAWEI CAM-L21 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…