Ni kawaida binti wa miaka 13 kuvunja ungo?

Ni kawaida binti wa miaka 13 kuvunja ungo?

Mfundisheni usafi.

Mfundisheni afya ya uzazi.

Mfundisheni mabadiliko atakayoendelea kuyaona.

Mtoto wa shemeji amevunja ungo mwezi wa 6 akiwa na miaka 12, darasa la 6.
ahsante sana!
 
mkuu kuharibiwa mtoto wa kike inakera zaidi. katika jamii zetu hizi za mfumo dume mtoto wa kiume akiharibu kwa jirani huko hata huumii sana (zaidi utakuwa na hisia za kufurahisha za 'udume' tu wa mtoto wako akilini)
Umenena ukweli. Yaani mama akiona kijana wake anafukuzia vibinti anafurahi kimoyomoyo lakini mama huyohuyo akiona binti yake aliyevunja ungo anashikwa nyonyo nakwambia hadi kwa mwenyekiti wa mtaa mtafika.
 
Habarini!

Huu ni mwaka wa 13 wa kuzaliwa binti yangu na yupo darasa la sita sasa.

Jana mama yake ananivujishia siri kuwa mtoto amekuwa (amevunja ungo).

Wadau, ni kawaida kwa binti wa miaka 13 kuvunja ungo au hii ni abnormality?!! Nilitarajia kuanzia 15 huko na kuendelea.

Uzoefu wenu tafadhali....
Ni sahihi
 
Umenena ukweli. Yaani mama akiona kijana wake anafukuzia vibinti anafurahi kimoyomoyo lakini mama huyohuyo akiona binti yake aliyevunja ungo anashikwa nyonyo nakwambia hadi kwa mwenyekiti wa mtaa mtafika.
Kweli kabisa
 
Yes wengine wanawahi zaidi ya hapo kutegemea na hormones zake zilivyo ni kawaida tu!,

au ma vyakula ya ajabu ajabu wanayokula ..ndio unakuta hata mtot wa kiume kuwa na maumbile ya "kike kike"
 
Yes wengine wanawahi zaidi ya hapo kutegemea na hormones zake zilivyo ni kawaida tu!,

au ma vyakula ya ajabu ajabu wanayokula ..ndio unakuta hata mtot wa kiume kuwa na maumbile ya "kike kike"
Ahsante kiongozi
 
Ni kweli ila shida ni kwamba ni wapuuzi mno kuelewa hilo mpaka yawakute
Uzuri ninkwamba siku hizi kuna sheria kali sana, kuna siku nilishuhudia mtu amekamatwa kwa kumuita binti wa shule mchumba, mama wa binti alicharuka akamkamata jamaa shingo bahati nzuri askari walikua karibu wakasogea wakaondoka na jamaa
 
Back
Top Bottom