Ni Kazi gani (Profession) ambayo ukiwa nayo au ukiifanya tu basi tayari umeshaachana kuwa na Mungu na unamtumikia Shetani?

Ni Kazi gani (Profession) ambayo ukiwa nayo au ukiifanya tu basi tayari umeshaachana kuwa na Mungu na unamtumikia Shetani?

Mzukulu

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2020
Posts
1,401
Reaction score
2,641
Nasikia kuna Kazi (Ajira) za Fani (Professions) fulani ambazo ukizifanya hizo hata kama uwe kila Siku unasali Kumuomba Mwenyezi Mungu hawezi Kukubariki kwani zina Dhambi ndani yake na pia zimekaa Kilawamalawama na huwezi Kuzifanya bila kwenda Kinyume kabisa na Maandiko ya Kiimani.

Kuna Mtu Mmoja aliniambia kuwa Wanaofanya hizi Kazi wao tayari Dhambi zao kila Siku zinajiongeza tu huko Mbinguni...

1. Kazi za Njiwa (Chawa) wa Makao Makuu Oysterbay mkabala na Kanisa la Mtakatifu Petro.

2. Kazi za Wamiliki Hospitali yao Kuu iliyo katikati ya Mwenge, Mikocheni na Kawe.

3. Kazi za Kuwaangalia na Kuwachunga wale walioanza Maisha yao ya Milele Tabata Segerea na Temeke Keko.

4. Kazi za kuwa Msahihisha Mitihani ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu hasa vile vyenye Wanafunzi wa Kike Warembo sana.

5. Kazi za kuwa Dalali wa Vyumba kwani unajua kabisa unapompeleka Mteja aishi ni njia Kuu ya Mafuriko katika Masika.

6. Kazi za kuwa Kondakta wa DalaDala kwani unakuwa unakataa Kupakia Wanafunzi ambao ukizeeka wanaweza Kukulea.

7. Kazi za kuwa Mwanasiasa kwani tokea Siasa zianze duniani hakuna Mwanasiasa ambaye 24/7 huwa anasema Ukweli.

Hizi ni zangu ila na Wewe Ndugu unaweza ukaziweka zako hapa ili wahusika wajijue na wasijisumbue Kumuomba Baba Mungu.
 
Tour guide.
Hutaenda church.
Utaaza kunywa wine kama utani hivi,
Siku nyingine utajaribu Gin and tonic ,
Siku nyingine utakunywa kili kama 6 hiv,
Ukirudi likizo utapiga kvant kama buku hivi,
Ukirudi kazini meneja atakufokea na utaamua
kupiga bangi kama 1kg hivi.
Utapenda sigara kama unavyopenda Kula.
Finally unakuwa wakala wa Lucifer kiutani utani tu
 
Dhambi hailetwi na kazi ni drive ya fikra na kamati na ubongo wako. Unaweza ukatenda dhambi hata kwa kujifungia ndani ya chumba chako kutoka asubuhi mpaka jioni.

Usipende kutumia maneno ya watu kama siraha ya kusimamishia madai yako. Tumia kichwa kufikiri 🤒🤒🤒🤒🤒
 
Usalama wa taifa. Utakuwa mnafiki na muongo, pia utapokea maagizo yasiyo ya haki uyatekeleze. Hii ni direct kwa shetani endapo utakuwa unapewa maagizo maovu

Hakimu/wakili/jaji/mwendesha mashtaka. Hawa wanaweza lazimishwa na serikali kumbambikia mtu kesi e.g ya uhujumu uchumi au drugs. Wakili anaweza tetea uovu ingawa ana option ya kukataa hivyo kuwa na wateja wachache mno. Wote wana chances nyingi za rushwa, uonevu na uongo.

Watoza ushuru/kodi/watoa vibari/ugavi. Hawa kila siku hufanya dhambi kazini kwa kutokuwa waadilifu. Mambo ya nifanyie mpango ndo dhambi zenyewe.

Wafanyakazi wa guest house/lodge na wamiliki. Hawa rohoni wanajua kabisa kinachofanyika, yani wanategemea mapato yao kwenye uzinzi. Kulala wageni mara nyingi si hata 30% ya mapato yote.

Polisi hasa traffic. Sjjawahi ona traffic sheikh mshikadini au mlokole. Hawa maisha yao ni udanganyifu na wizi, dhulma.

Kazi ambayo ina chance ndogo ya dhambi ni ualimu. Hii inaweza ambatana na baraka kama mtu anapenda wanafunzi hasa watoto wadogo. Waalimu ndio watu wa kawaida ambao wakifa watu husikitika. Na hawaumwi magonjwa ya ajabu ovyo, kumbuka ndo waajiriwa wengi zaidi.

Anyway, tufanye kazi yoyote ile iliyo rasmi kwa uadilifu.
 
Tour guide.
Hutaenda church.
Utaaza kunywa wine kama utani hivi,
Siku nyingine utajaribu Gin and tonic ,
Siku nyingine utakunywa kili kama 6 hiv,
Ukirudi likizo utapiga kvant kama buku hivi,
Ukirudi kazini meneja atakufokea na utaamua
kupiga bangi kama 1kg hivi.
Utapenda sigara kama unavyopenda Kula.
Finally unakuwa wakala wa Lucifer kiutani utani tu
Aisee!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usalama wa taifa. Utakuwa mnafiki na muongo, pia utapokea maagizo yasiyo ya haki uyatekeleze. Hii ni direct kwa shetani endapo utakuwa unapewa maagizo maovu

Hakimu/wakili/jaji/mwendesha mashtaka. Hawa wanaweza lazimishwa na serikali kumbambikia mtu kesi e.g ya uhujumu uchumi au drugs. Wakili anaweza tetea uovu ingawa ana option ya kukataa hivyo kuwa na wateja wachache mno. Wote wana chances nyingi za rushwa, uonevu na uongo...
Indeed

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh nimesoma comment za wadau mbona kazi zote zimetajwa
Duh ni hatar
 
Back
Top Bottom