Ni kero gani ambayo ushawahi kukutana nayo wakati unatafuta nyumba ya kupanga?

Ni kero gani ambayo ushawahi kukutana nayo wakati unatafuta nyumba ya kupanga?

Wakuu,

Hata kama umeshashusha mjengo watu wengi huwa wanapanga sana chumba au nyumba

Sasa kabla ya kupata nyumba ya kuishi kunakuwa na ile process ya kuipata hiyo nyumba

Siku hizi kila kona kuna madalali na mimi hawa ndo wananikera sana.

Kuna wakati nilikuwa natafuta nyumba nilizungushwa mno. Can you imagine dalali unahangaika nae wiki mbili kila siku anakuambia nimepata nyumba sehemu ukienda nyumba haina viwango na ni lazima umpe hela kama 10k kila anapoenda kukuonesha nyumba mpya.

Kiukweli nilikuwa nakwazika sana.

Nyie wenzangu vipi? Mkitafutaga nyumba huwa mnakumbana na changamoto gani?

View attachment 3456286
Madalali me ndo kero yangu kubwa, na sijawahi kuelewa kabisa, yaani bidhaa ni yako lkn Ili unioneshe bidhaa yako napaswa me kukulipa ati hela ya nauli 🤗
 
Back
Top Bottom