nakumbuka nikiwa darasala nne mama alikuwa natabia ananunua pipi nyingi kila akienda sokoni anatupa na nyingine anahifadhi kwenye kamkoba chake anaweka kwenye droo ili ukifanya vizuri kazi au shuleni anakupa pipi kama pongezi, sasa mimi nikawa naenda kuiba mama akawa anajua,,... nikaanza tabia ya kuzifungua nazinyonya narudisha kwa zamu maza akiuliza mbona hizi pipi zinaloa anakosa jibu.. sku hiyo akawa kama anahisi jambo haliko sawa nikaingia kama kawaida chumbani kwa mama ile kufungua mkoba wake nikavunja kifungo cha mkoba nikaanza kazi ya kuzinyonya kwa zamu na kurudishia kumbe mama yupo dirishani anasoma mchezo ..jamani nilifungiwa mule chumbani kama mtu anajua fimbo za mueleimu alikata nyingi milipigwa kama kibaka kuanzia sa kumi mpaka sa moja mdingi aliporudi nakukuta madogo wanalia mlangoni ndiyo pona yangu.. mpaka leo yale mapipi nikiyaona hamu sinaga nayo