Tuwakumbushe Wanajeshi wetu hasa Jeshi la Wananchi wa Tanzania .
Jeshi letu sio Jeshi la Familia ya mtu mmoja.
Jeshi letu sio Jeshi la kulinda maslahi ya MTU mmoja na familia yake na marafiki zake anaowateua na kuwapa vyeo ili wale maisha. Ndio maana anasema nitakuteua mana nafasi zipo.
Jeshi letu sio la kuwalinda wezi wa Mali za umma walijificha ndani ya CCM tangu Uhuru. Watu waliofilisi mashirika ya umma na kujilimbikizia mali nyingi kila mahali. Ukiona majengo Mengi Kwenye miji yote kama sio ya NSSF,PPF basi yana mikono ya wanasiasa wa CCM. Sasa wanafanya kila hila watumia majeshi yetu kukalia madaraka.
Jeshi letu sio Jeshi la Kikabila,yaani la mtu mmoja kutaka kujiweka chini ya huruma ya Ukabila na kutumia dola kuhalalisha Shindi haram kwa Chama Chochote.
JESHI LETI NI JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA.
Jeshi Letu lipo kwa ajili ya wananchi wote wa Tanzania .
Wakati Mwingine Jeshi la polisi linakaa kisiasa siasa kulingana na maslahi binafsi . Mfano OCD au RPC ,Mara RTO ,Mara RCO Mara OCCID mara OCS ; Nafasi zote hizo ni nafasi zenye kupata marupurupu na rushwa za hapa na pale lakini pia ni nafasi zenye maamuzi makubwa ya kuweza kuwanyima haki watu hivyo wananchi hasa wanye biashara wanajipendekeza kwa hizo nafasi za kipolisi.
Hivyo Tunaliomba Jeshi la wananchi wafanye Uchunguzi kimya kimya mana wana itelijensia imara sana ili wajiridhishe kuwa kamapeni zinafanyika kwa usawa au laa, lakini pia uchaguzi utafanyika kwa haki au laa. Wajiridhishe kuwa kama CCM itashinda basi ishinde kwa Haki na itangazwe na wapinzani watakaoshindwa kwa haki wakubali matokeo.
Kuna watu ni Rahisi sana kuhongwa na Wagombea au kuahidiwa hizo nafsia zenye maslahi ndani ya Polisi na kutumika kuvuruga kura za wananchi wanaoweka viongozi wao.
Jeshi letu la wananchi wa Tanzania liwaangalie na kuwachunguza kwa makini sana ili Watu wachache kwa tamaa zao wasitumike kuvuruga amani ya nchi.
Naamini wakuu wa Jeshi wapo Makini sana na hawakufikia vyeo vye Ujenerali kwa Hisani ya Polepole na Bashiru Bali kwa weledi wao na uwezo wao na uzalendo wao katika kulitumikia Jeshi na wananchi wa Tanzania ,hivyo kuwaua watu ili kumfurahisha Polepole na Bashiru watu waiookotwa Jalalani litakua jambo la kusikitisha sana na dhambi kubwa kwa Mungu.
Yani Bashiru na Polepole wameibuka tu Juzi na midomo yao tu halafu wawaamrishe wanajeshi na polisi walioko kwenye kazi ya hatari na yenye kuhitaji utulivu na maamuzi ya haki ili kuepusha amani kutetereka kwa kuiba kura na kumtangaza mtu atakayeshindwa na kumwacha aliyeshindwa.
Lakini kama CCM itashindwa basi Jeshi letu Lisijiingize kuwatetea Wezi waliokataliwa na Wananchi ambao ndio wenye Jeshi.
Jeshi la wananchi watakapobaini kuwa CCM imeshindwa ila inatumia Polisi wanye maslahi binafsi kuwapiga na kuwaua wananchi basi lisisite kuwarudisha Polisi Nyumbani haraka na kuwaacha wananchi wakashangilia ushindi wao kwa haki.
Ndio maana Maafisa wengi sana wa Jeshi ni Watu wanaopenda sana Dini na kumtii Mungu kwa dhati. Ndio maana Jeshi letu linaheshimika sana mana halijaegemea upande wa Chama Chochote cha siasa zaidi ya kulinda mipaka ya nchi yetu na amani ya Taifa letu wakati wa dharura hasa serikali inaposhindwa kutimiza majukumu yake sawasawa.
Hata wastaafu wengi wa Jeshi ni watu wenye Amani sana na Wananchi kwa sababu wanajua thamani ya wananchi na walipa Kodi.
Mwaka Huu ni Uchaguzi wa Rais ,wabunge na madiwani,
Rais anatakiwa awe mmoja Tanzania na Zanzibar mmoja.
Wamegombea wengi na kila mmoaja ana watu wanaoamini kuwa mgombea wao ndiye anayefaa.
Wote muda huu wamepewa miezi miwili ya kuomba Kura. Kuna mmoja ambaye amekaa madarakani kwa miaka mitano. Naye pia anaomba tena kazi ya kuongoza nchi ya Tanzania sio kupitia Jeshi wala Tume wala Polisi wala Chama Bali kupitia KURA za watanzania ambao ndio wanaolipa kodi ili akae ikulu na kusimamia mipango iliyowekwa Tangu tulipopata Uhuru.
Kwa hiyo yeyote atakaye shinda iwe ni Ubunge au Urais au Udiwani basi atangazwe mapema ili kuepusha vurugu.
Polisi nao waache kufanya kazi kwa kuendekeza ubinafsi na kujipendekeza mana wanavuruga ustaraabu wa watanzania waliopata Uhuru kwa amani.
Tumeona Maeneo yote ya Ukanda wa Ziwa ambapo watu walidhani kuwa labda kuna Ukabila umeanza kujijenga watanzania wamekataa kufanya siasa za kikabila .
Wale wapumbavu waliokua wanasema ni zamu yetu wameaibika mana wao waliwaza vyeo na madaraka na uteuzi kikabila wakati wananchi wa Tanzania ni wamoja na hawabaguani ndio maana wamonekana kumkubali Lisu toka Singida kuliko Jirani yao wa Chato iliyokua Kagera zamani.
Potelea mbali ni bora basi kama Wataiba kura halafu waongoze nchi kistarabu na kwa amani na upendo na kuheshimu hata wale waliowaibia lakini wanaiba kura halafu wanaongoza kwa jesuri ,visasi,majivuno ,ubabe,kiburi,dharau, vitisho, na kila aina ya unyanyasaji.
Kwa kweli atakayeshindwa adhibitiwe ili asije akatumia nguvu kutangazwa. Hata kama ni Raid wetu Mpendwa JPM akishindwa akubali tu na kuridhika na apumzike ili nchi isiwe na mtafaruku. Nchi ni kubwa kuliko yeye . Na uzima na uhai wa kila mtu ni muhimu kama ulivyo wa mtu mwingine . CCM ni Chama cha watanzania kama kilivyo Chauma ,CUF ,Chadema na ACT. Wote wanaomba uongozi atakayepata kura nyingi ndiye atakayetangazwa.
Mungu Bariki Jeshi Letu la Wananchi wa Tanzania ili lisije likageuka kuwa Jeshi la mtu au kakundi kwa watu wenye maslahi ya kwao na familia zao.