Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
I'll never forget such kind of moment in my life. Ile wamepika matoke wakayachanganya na maharage, plus matumbo ya ng'ombe, karanga za kusiginwa plus karanga za kutafunwa, humo humo mfuru, kha! Ile siku nilitembea kama naruka majoka vile kuelekea toy kujiharishia, tena mbele ya mama mkwe na madada wa muke wangu
Choo kilikuwa na katundu ka kuchungulia nje ukiwa umechutama, nikitamani waondoke nianze yangu, lakini ndo kwanza wako kwenye kijikeka mbele ya choo. Ile kuchutama tu, walisikia Buuuuuuuum Bhaaaaa Pah! Kila mmoja wao alikuwa mbele ya tukio alikimbia kama mchwa kichaa, mama mkwe alikimbia akiwa ameweka mikono kichwani huku akiuficha mbichwa, wakina dada walikimbia huku wameziba midomo yao ili kuizuia cheko, mke wangu pekee ndiye aliyebaki eneo la tukio akivumilia hali ile ya milipuko ya mabomu ya Mbagala kwa huruma nyingi mno
Nilivyotoka tu chooni, niliwasha bolt nikaondoka zangu, mke wangu alinifuata akiwa na virago vyetu. Huo ndo ulikuwa mwisho wa kutembelea ukweni
Mola awabariki sana wake zetu
Ila mtoto wa mama mkwe atakuja kuua jitu humu ndani