sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,406
- 19,375
Binafsi nakumbuka kuna kipindi maisha yangu hayakuwa tofauti sana na ndege, sikuwa na mipango kabisa, Nikiamka ndio ntajua cha kufanya na nlichofikiria kufanya kwa asilimia kubwa kilihusisha mambo ya upumbavu wa ujana kama kutilia nguvu kubwa ishu za madem, kubeti, kupiga stori ili siku iishe, n.k.
Ila kuna siku nikawa nachana nywele kwenye kioo baada ya kumaliza nikaanza kujiangalia kwenye kioo sijui ni kitu gani kilitokea nikaanza kuongeleshana na mimi mwenyewe, Nikaanza kujiongelesha huku nikijitazama.
Nilijiuliza umri umeenda sasa, umri nilionao vijana wenzangu kutwa nzima nawaona wanawahi kuamka kwenda kujitaftia riziki huku mimi naamka saa tatu na hakuna cha maana nachofanya.
Nilijiuliza mimi na wale wenye magonjwa waliyopata kwasababu ya zinaa tuna tofauti gani ikiwa mimi ni mtu na wao ni watu,
Nikajiuliza bado nipo kwa wazazi tu kwa umri nliokuwa nao japo nlikuwa kijana mdogo lakini kuna wenzangu walikuwa wanajitegemea
Ni vitu vingi nilijuiliza.
Baada ya hapo nakumbuka ile siku nlilala sita usiku, Kesho yake niliamka saa 12 asububuhi kufanya usafi home hadi wakanishangaa na ndio ikawa tabia kuanzia hapo.
Haikuchukua muda sana nikapata hasira ya kutafta kazi, nilitafta sana nikakosa, Nilikuwa na visenti nikakodisha frem ya elf 50 kwa miezi mitatu, Nikawa nakaanga chipsi nyumbani naziweka kwenye hot pot kubwa naenda nazo kwenye fremu basi nikawa napata visenti.
Akili ikawa imebadilika saizi sikuwa nashinda mtaani na mambo ya madem sikuwa na mda nayo nilitulia na mmoja tu.
Basi maisha yakaenda nilifanya interview nyingi na nikabahatika kuajiriwa serikalini,
Hakika nisingeacha mambo ya kitoto hali ingekuwa mbaya