Thecoder
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 1,590
- 4,244
Wasalaam...
Ni marufuku kuongea juu ya jambo lolote kabla ya kufikiri ila pia fikra haziji kwenye kichwa kisicho na maarifa juu ya jambo au mambo yazungumzwayo.
Kwahiyo ili mtu apate uwezo mzuri wa kufikiri zaidi ni lazima ajiongezee maarifa ya hapa na pale ndani ya kichwa chake na njia moja wapo ya kuongeza maarifa ni kusoma vitabu mbalimbali.
Kwa maana ndani ya vitabu huwa tunajifunza juu ya mambo mbalimbali yaliyofanywa na watu wengine pamoja na matukio ya hapa na pale ambayo yaliwahi watokea watu wengine na namna ambavyo waliweza kukabiliana nayo.
Lakini pia ndani ya vitabu tunapata hamasa kwa maana tunasoma mafanikio ya watu wengine katika biashara kadha wa kadha kwahiyo kupitia hamasa hizi na sisi zinatufanya tujitajidi katika utafutaji.
Mimi mwaka uliopita nilisoma soma vitabu kadhaa ila kitabu ambacho nilimaliza nacho mwaka ni the fastlane millionaire kilichoandikwa na ndugu MJ DeMarco.
Sasa tuambie na wewe, ni kitabu gani ambacho ulikisoma na kikakupa funzo fulani au kikakuhamasisha kwenye jambo fulani na ungetamani na wengine wakisome?