Ni kitu gani ambacho hupendi kukifanya katika maisha yetu ya kila siku lakini unafanya kwakuwa huna namna

Ni kitu gani ambacho hupendi kukifanya katika maisha yetu ya kila siku lakini unafanya kwakuwa huna namna

Sipendi kuona watu wanakosa amani na kupata shida wakati Mimi nipo.
Napenda kuwa faraja kwa watu japo kuna wakati najikuta nashindwa kutekeleza hilo jukumu
 
Sipendi tabia yangu ya kuwa na huruma kupita kiasi.
Imenigharimu mambo mengi sana,kuna muda imeniingiza hadi kwenye madeni nikamhurumia mtu na kwenda kumkopea hela kwa mtu.
Kuna muda nilishashinda na njaa ili mwingine ale na bado akanilaumu
Kuna muda huruma ilinifanya nionekane mpumbavu
 
Sipendi kabisa kuhudhuria sherehe
Kipindi nipo shule nimewahi kuhudhuria hafla moja tu!nayo nilienda kwa kulazimishwa..nje na hapo sijawahi gusa kwenye bday party ya mwana praise mwenzangu hata mmoja.
 
Sipendi kusafiri.
Huwa nasafiri basi tu unakuta Safari ni ya lazima.
Safari ikikaribia nawaza hadi nakonda.

Sipendi kuongea na simu.
Kuna muda inaweza iite na nisipokee na ninaiona kabisa.
Mara moja moja sana nalazimika kupokea.
Napenda kusafiri pembeni yangu akae mwanaume mrefu mpole mpole lkni mchangamfu😉😉😉safari itakuwa fupi..

Kuna vitu vitabadilika taratib kabisa mama
 
Sipendi kwenda ugenini
Huwa naenda tu kwa Sababu Hakuna namna.
Kuna kipindi nilienda sehemu yaani nilikuwa mnyonge mno hadi nadhani wenyeji walijisikia vibaya..siku 2 nilizokaa niliona kama mwaka.
 
@Chakorii, again[emoji28][emoji28]

Hapo kwenye kuvaa kyupi tupo wengi, mimi sipendi naona tu kama iniwekea uzio, nikiwa nyumbani sivai kabisaaa labda niwe natoka au siku niamke na mood ya kuvaa

Sipendi pia kuosha vyombo na kupasi surali za Mr, yani naona kama ni kazi inayonifanya nijiskie naonewa sema tu sina jinsi inabidi nifanye

Sipendi pia kutoka au kuzurura kama Saint Anne, tena kama nipo likizo naweza kukaa ndani tu hata nje ya geti sitoki kama mwali
Ndio mama...🧚‍♀️🧚‍♀️🧚‍♀️...

Nilijua kutokuvaa kufuli ni mimi peke yangu loh..ila huyu mjamaa asipovalishwa kyupi a nafurahi sana😅😅🙈🙈🙈

😅😅ndio hivyo lkni tunakuwa hatuna mnama...ni kuendelea kufanya vile tusivyovipenda ila maisha mengine yapste kwenda.

Nimefurahi kukuona tena madame Mtende
 
nna rafiki yangu ye hua analoweka nguo siku 3 then anasuuza na kuanika anasema zishajifua[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Tobaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Huyo hawezi ishi nyumba yenye watoto hat wawili tu ambayo kufua ni ratiba ya kila siku kama ilivyo ratiba ya kula.
 
Napenda kusafiri pembeni yangu akae mwanaume mrefu mpole mpole lkni mchangamfu[emoji6][emoji6][emoji6]safari itakuwa fupi..

Kuna vitu vitabadilika taratib kabisa mama
Safari sidhani kama nitakuja kupenda
 
Back
Top Bottom