Ni kitu gani cha kijinga ulichokifanya uliposhika hela nyingi kwa mara ya kwanza?

Ni kitu gani cha kijinga ulichokifanya uliposhika hela nyingi kwa mara ya kwanza?

wewe jamaa ulistahili tuzo ya "ubazazi".
maana matendo yako yote ukishika hela
akili yote inahamia uko "centre of gravity".
Hahaha! Mkuu, hela za ghafla huwa zinachanganya sana ukiwa na mawazo mafupi, unakuwa unatamani kujaribu kila kitu. Ila kwa sasa Nimebadilika sana mpaka Najishangaa.
 
Nilinunua shart 2 kwa laki. Adi siamin min kilnpata sukuile maanake sikua ata nimelewa
 
Hahahahahahaha
Mie mpaka leo nikikumbuka najuta sana maana Nililala na madada wanaonizidi umri watatu kwa siku moja na kunywa vilevi vikali siku inayofuata na kulala kwenye mtaru nilishituka saa mbili asubuh tena kwa kushituliwa na watu wakijuwa nimekufaa,,,yani ndani ya siku mbili nikawa nimeshamaliza mil 1000,000/-,,Yani nikikumbuk huwa naumia sana
 
Sita sahau,tulivyopewa mgao wa urithi kila mrithi alipewa milioni ushirini...mm niliwaomba benki hela yangu iwe ni ya chenjichenji yote..basi wakanipa coins za mimia za shilingi milioni 20,mpaka leo ninazo huwa natumia shs 300 kwa siku.ili zisiishe haraka.
 
Boom hilo Piga pombe mbaya na mademu baada ya wk nikafulia nkawa mpole hatari
 
Mimi mkuu baada ya kupata m 5 nilizokopa banki nilimpa kaka yangu tufanye biashara yeye akenda dubai kununua nguo baada ya kurudi tu akahama nchi akaelekea msumbiji hadi leo sina mawasiliano.naye na hatujaonana ni miaka 3 sasa na deni bado nadaiwa bank.niliumia san
pole sana mdau
 
Nilisafiri mkoani kumfuata mwanamke Niliekuwa Nikiota kumpata mpaka Nikawa Naumwa. Tulitumbua raha kwa kuhama hoteli kadhaa za kifahari mkoa ule. Yaani ilikuwa Tukichukua chumba halafu Tv ikazingua au channel za Movies hazieleweki, kesho yake Tunatafuta hoteli kali zaidi na kitu cha kwanza kukagua ni Channels na ndipo mengine yanafuata. Yaani hadi leo huwa Nadata sana na huyu mwanamke maana siinjoi hata kinywaji Nikikumbuka navyoinjoi kunywa nae. Nikarudi Dar bado haikutosha, Nikamtumia Nauli, breki ya kwanza Ilikuwa mitaa fulani inayoongoza kwa Bar na ukahaba hapa Dar ambako Tulikaa kwenye lodge moja kali sana kwa kama siku saba mfululizo Tukitoka night tu. Pesa inazuzua sana usipotulia ingawa binafsi Nachokumbuka ni matukio Niliyowahi kufanya kwa namna ya hatari sana kwa sababu sikumbuki mara ya kwanza kushika pesa nyingi aisee. Huyu Tuliefanya nae hizi vurugu ni mama wa baby wangu sasa na bado yuko ndotoni mwangu, it feels stupid and crazy sometimes.
Kituko kingine Nilichowahi kufanya ni kumfuata msichana kampala ambako Tulitumbua pesa kama vichaa pia kwa wiki mbili. Ingawa Nilikuwa Naishi mwenyewe, Nahisi kosa nililofanya ilikuwa kutomuaga mtu yeyote katika familia yangu.
Kituko kingine Nilichowahi kufanya ni kile Nilichokifanya baada tu ya kutoka kuchukua pakee ya mgao wangu, Nikaenda Tigopesa, Airtel money na M-pesa Nikazijaza laini zote na pesa full. Nikabakiza kama M 1.5 mfukoni, Nikavuka na pantoni kigamboni kuja town. Hapo niko raugh kweli kweli, Nikamchukua taxi driver Nikamuuliza gharama ya kutoka pale hadi Bagamoyo ambako Nilimtanguliza mtu, aliponipa bei, Nikamwambia Tupite Sinza Nijafanye Shopping mpaka ya begi Nikatafuta lodge Nikaoga na kuchange, kisha Tukanyoosha mpaka Bagamoyo. Kilichotokea ni kuwa pamoja na mbwembwe zote hizo, Tuliishia kutibuana na alienisubiri halafu Nikaharibu zaidi baada ya kutongoza mtu mwingine kwa hasira. In short Tuliishia kulala vyumba tofauti na kurudi kila mtu na njia yake. Ila utoto ndio uliochangia kwa kiasi kikubwa.
Nina visa vingi ila hebu wengine wachangie.
Dah!! We jamaa hatari sna, kma ikitokea nkafanya vtuko vyote ivo, atasijui ntawezaje kujisamehe
 
Back
Top Bottom