Ni kitu gani cha kijinga ulichokifanya uliposhika hela nyingi kwa mara ya kwanza?

Nilinunua raba za all-star za rangi kama 6 hivi tofauti kwa wakati mmoja
 
Ilikua hela ya NSSF 2.5 m nikaongezea laki 5 nikanunua Kiwanja Mwanza-Kabusungu
Kama ulinunua kiwanja cha pesa hiyo Kabusungu basi kweli hicho ni kitendo cha kijinga 108%
 
Ulimpa zote???
 
Nilivuka mto hatari sana unaoenda kasi,
sharti kubwa utembee kwa kutanua miguu majini, unapovuka mkuu. yaani maji mengi ya shingo! ukikanyaga kibonde kidogo tu down umeenda! ili kufika ng'ambo ya pili ya mto palipo na dawa,

Lengo langu nika mloge mtu wangu aliyenotoroka arudi tuishi! kilicho nisikitisha ni kuwa wala hata hakurudi ndo kwanza kabebwa na mwingine.

Na mtu niliye kuwa namhangaikia mbaya zaidi kuliko yote hana kazi, hana hela, hana Elimu, Hata ile ya Darasa la saba tu, mwandiko wake ni kituko, kusoma hajui, yaani ni mzigo kwa kwenda mbele!
 
Hapana Mkuu, Hospitali ya wilaya ya Ilemela ipo karibu na hapo na imeanza kufanya kazi, ipo pia miradi kibao ya maendeleo hapo. Hongera sana Mkuu!
Kuna yapi mapya zaidi ya Hospital boss?
 
Nakumbuka nikiwa form two alikuja pinda,enzi hizo yupo ofisi ya rais na sio waziri mkuu.

Walipofika nikapewa maiki kukaribisha wageni na kuelezea shule yetu kwa kifupi kwa lugha ya wenzetu.

Basi mzee nikajipinda pale,ulimi ukanyooka fresh maana taarifa nilipewa mapema ili nijiandae .

Basi pinda akavutiwa na jinsi nilivyowasilisha na nilivyokuwa natembea kwa madaha ,Pinda akajua hiki kichwa kinajua lugha kumbe mimi nmekesha siku mbili kwenye kioo nikifanya mazoez.

Akanipa ef20.hiyo ef 20 nilinunua mandazi ,vibama na bagia wanangu wakawa wananiita kibopa,

Kufika jioni nina ef7,nikaenda kununua viatu vya mpira wa miguu viliandikwa cosovo,sisi tuliviita njumu.

Nilijuta sana maana siku zote nilikuwa nataman kununua viatu vya basketball vya ef20 mtumban ,ila nilipopata pesa nikasahau nikaishia kununua njumu
 
Kuna yapi mapya zaidi ya Hospital boss?
Kuna vyuo vtajengwa hapo, pia nilisikia watajenga gereza huko...kuna rafiki yangu alilipwa fidia ya eneo lake hapo ila nimeshahu ni taasisi gani ya serikali itajengwa hapo
 
Atiii vibama nimecheka balaaaaa
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†Huyo mbuzi mwache tu ale majaniπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…