Ni kitu gani cha kijinga ulichokifanya uliposhika hela nyingi kwa mara ya kwanza?

Ni kitu gani cha kijinga ulichokifanya uliposhika hela nyingi kwa mara ya kwanza?

Nilisafiri mkoani kumfuata mwanamke Niliekuwa Nikiota kumpata mpaka Nikawa Naumwa. Tulitumbua raha kwa kuhama hoteli kadhaa za kifahari mkoa ule. Yaani ilikuwa Tukichukua chumba halafu Tv ikazingua au channel za Movies hazieleweki, kesho yake Tunatafuta hoteli kali zaidi na kitu cha kwanza kukagua ni Channels na ndipo mengine yanafuata. Yaani hadi leo huwa Nadata sana na huyu mwanamke maana siinjoi hata kinywaji Nikikumbuka navyoinjoi kunywa nae. Nikarudi Dar bado haikutosha, Nikamtumia Nauli, breki ya kwanza Ilikuwa mitaa fulani inayoongoza kwa Bar na ukahaba hapa Dar ambako Tulikaa kwenye lodge moja kali sana kwa kama siku saba mfululizo Tukitoka night tu. Pesa inazuzua sana usipotulia ingawa binafsi Nachokumbuka ni matukio Niliyowahi kufanya kwa namna ya hatari sana kwa sababu sikumbuki mara ya kwanza kushika pesa nyingi aisee. Huyu Tuliefanya nae hizi vurugu ni mama wa baby wangu sasa na bado yuko ndotoni mwangu, it feels stupid and crazy sometimes.
Kituko kingine Nilichowahi kufanya ni kumfuata msichana kampala ambako Tulitumbua pesa kama vichaa pia kwa wiki mbili. Ingawa Nilikuwa Naishi mwenyewe, Nahisi kosa nililofanya ilikuwa kutomuaga mtu yeyote katika familia yangu.
Kituko kingine Nilichowahi kufanya ni kile Nilichokifanya baada tu ya kutoka kuchukua pakee ya mgao wangu, Nikaenda Tigopesa, Airtel money na M-pesa Nikazijaza laini zote na pesa full. Nikabakiza kama M 1.5 mfukoni, Nikavuka na pantoni kigamboni kuja town. Hapo niko raugh kweli kweli, Nikamchukua taxi driver Nikamuuliza gharama ya kutoka pale hadi Bagamoyo ambako Nilimtanguliza mtu, aliponipa bei, Nikamwambia Tupite Sinza Nijafanye Shopping mpaka ya begi Nikatafuta lodge Nikaoga na kuchange, kisha Tukanyoosha mpaka Bagamoyo. Kilichotokea ni kuwa pamoja na mbwembwe zote hizo, Tuliishia kutibuana na alienisubiri halafu Nikaharibu zaidi baada ya kutongoza mtu mwingine kwa hasira. In short Tuliishia kulala vyumba tofauti na kurudi kila mtu na njia yake. Ila utoto ndio uliochangia kwa kiasi kikubwa.
Nina visa vingi ila hebu wengine wachangie.
Duuh hii kali sana
 
Mimi sio cha kijingaa iyoo ya kwanza baada ya kushinda Bahati nasibu ya TBL kipindi kilee cha Nsekela nilisafiri mpaka mkoani anakoishi Dada na kumpa Mtaji Wa biashara..sasa umri wangu Wa miaka 20 ivi haikumjia kuamini Dada Angu kama nampa tu Maburungutu ivi ivi Kwa shauku aliniuliza he Ni mkopo?nikamjibu hapana hakuamini..na nilifanya ivyo nikiwa Chuo na mahitaji mengi sema kilichokuwa kinaniuniza ni ile halii aliyokuwa ya kuteseka watoto 6,baba hakuna hana kazi ilichangia nifanye vile..but sadly enough baada ya kufanikiwa na kujengaa baadae through biashara aliyoianzisha ilikuja kutokea Bibi akafariki ikabidi wajukuu turithi nyumba Dada akisaidiana na mtoto Wa mamdogo waliuza nyumba Milioni 150....Dada yanguu huyoo Wa pekee alinigawia milioni 4 tu..na yeye kujinunulia nyumba nyingine...kwani wazazi woote walifariki ivyo wajukuu ndo tulirithishwa..OK.ni mengi I'm sorry to say all these..ila nimejifunza mengi sana..
Mmh pole sana, kiukweli binadamu wengi tuna roho mbaya na ubinafsi uliokithiri, Ila basi tu, kasahau ule wema woote uliomtendea, ur success ndo itakuwa best revenge @sweetapple
 
Mimi namshukuru mungu,mara tu baada ya kumaliza chuo nilipata kazi katika taasisi fulani ya serikali ambapo nilipata bahati ya kusimamia utekelezaji wa mradi fulani hivi wa jamii, kwa kweli mradi ule ulikuwa na hela nyingi sana tofauti na za utekelezaji husika. Ilitokea kupata fedha nyingi sana kutokana na utekelezaji wa mradi ule, ila ninachomshukuru mungu sikuwa mfujaji wa pesa ingawa starehe za hapa na pale nilikuwa hazinipiti, nilinunua kiwanja na nikaanza kujenga mjengo, kweli mpaka mradi unaisha nami nikawa nimeweza kukamilisha mjengo wangu ila nilibakiza vitu vidogo vidogo kama kupiga ceiling board. Sasa mradi umeisha ilikuwa ni ngoma kuimalizia sehemu iliyobakia kwani nilikuja gundua kuwa mishahara hii inayolipwa ni midogo sana ukizingatia na hizi extended familia zetu ndio bhasi, lkn namshukuru kwa hicho kidogo ambacho nilikipata tofauti kama ningekuwa nimekunywa pombe na kuwanunulia nguo malaya wasiokuwa na shukrani hapa duniani, mbona ningejinyonga wakati huu wa ukata aisee!!!
 
Ha haaa njoo unipe mahela
Wewe mtoto! Ungejua unavyonipa hamu! Uko serious lakini?Kama uko serious,ngoja Nimalizane kwanza na Madame B maana yeye ndie alie kwenye financial plans zilizopo. Ameniahidi kuwa sitajutia, sijui wewe unaniahidi nini?
Sema kabisa maana sisi wengine huwa hatutanii wala kutaniwa. Niahidi kitu kizuri kizuri. Hela utapata, kwa hilo usihofu.
 
Wewe mtoto! Ungejua unavyonipa hamu! Uko serious lakini?Kama uko serious,ngoja Nimalizane kwanza na Madame B maana yeye ndie alie kwenye financial plans zilizopo. Ameniahidi kuwa sitajutia, sijui wewe unaniahidi nini?
Sema kabisa maana sisi wengine huwa hatutanii wala kutaniwa. Niahidi kitu kizuri kizuri. Hela utapata, kwa hilo usihofu.

Uwiii nimeghairi bana... Sina cha kukuahidi mie
 
Hahahahaaa ndo mwachane na wizi..
Usinicheke maana kila nikikumbuka natamani nikaseme kwamba mimi ndiye niliyeiba lkn hela yenyewe ishabwa,aliyeipata atakua yupo mbali kama ana plan za maana.
 
Back
Top Bottom