Nilisafiri mkoani kumfuata mwanamke Niliekuwa Nikiota kumpata mpaka Nikawa Naumwa. Tulitumbua raha kwa kuhama hoteli kadhaa za kifahari mkoa ule. Yaani ilikuwa Tukichukua chumba halafu Tv ikazingua au channel za Movies hazieleweki, kesho yake Tunatafuta hoteli kali zaidi na kitu cha kwanza kukagua ni Channels na ndipo mengine yanafuata. Yaani hadi leo huwa Nadata sana na huyu mwanamke maana siinjoi hata kinywaji Nikikumbuka navyoinjoi kunywa nae. Nikarudi Dar bado haikutosha, Nikamtumia Nauli, breki ya kwanza Ilikuwa mitaa fulani inayoongoza kwa Bar na ukahaba hapa Dar ambako Tulikaa kwenye lodge moja kali sana kwa kama siku saba mfululizo Tukitoka night tu. Pesa inazuzua sana usipotulia ingawa binafsi Nachokumbuka ni matukio Niliyowahi kufanya kwa namna ya hatari sana kwa sababu sikumbuki mara ya kwanza kushika pesa nyingi aisee. Huyu Tuliefanya nae hizi vurugu ni mama wa baby wangu sasa na bado yuko ndotoni mwangu, it feels stupid and crazy sometimes.
Kituko kingine Nilichowahi kufanya ni kumfuata msichana kampala ambako Tulitumbua pesa kama vichaa pia kwa wiki mbili. Ingawa Nilikuwa Naishi mwenyewe, Nahisi kosa nililofanya ilikuwa kutomuaga mtu yeyote katika familia yangu.
Kituko kingine Nilichowahi kufanya ni kile Nilichokifanya baada tu ya kutoka kuchukua pakee ya mgao wangu, Nikaenda Tigopesa, Airtel money na M-pesa Nikazijaza laini zote na pesa full. Nikabakiza kama M 1.5 mfukoni, Nikavuka na pantoni kigamboni kuja town. Hapo niko raugh kweli kweli, Nikamchukua taxi driver Nikamuuliza gharama ya kutoka pale hadi Bagamoyo ambako Nilimtanguliza mtu, aliponipa bei, Nikamwambia Tupite Sinza Nijafanye Shopping mpaka ya begi Nikatafuta lodge Nikaoga na kuchange, kisha Tukanyoosha mpaka Bagamoyo. Kilichotokea ni kuwa pamoja na mbwembwe zote hizo, Tuliishia kutibuana na alienisubiri halafu Nikaharibu zaidi baada ya kutongoza mtu mwingine kwa hasira. In short Tuliishia kulala vyumba tofauti na kurudi kila mtu na njia yake. Ila utoto ndio uliochangia kwa kiasi kikubwa.
Nina visa vingi ila hebu wengine wachangie.