Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Niliwahi kuwa na rafiki ambaye tulikuwa karibu sana kipindi tukiwa chuo. Sasa kuna siku niliibiwa simu ikabidi nitamtafute mpenzi wangu kupitia simu yake nimpe taarifa. Nikaja kununua simu lakini baadae nikaanza kugombana sana na mpenzi wangu, yaani ugomvi kila kukicha. Nikachunguza nikaja kugundua kuwa rafiki yangu ndo anamwambia mambo yangu na mengine yalikuwa ya uongo.
Sikumwambia chochote nikamcut off nikaendelea na mambo yangu hadi leo sijawahi kumwambia sababu na yule mpenzi na yeye nikaachana nae ila tukaendelea kuwa marafiki. Siku kadhaa zikapita yule Ex akarudi ananiomba msamaha turudiane na amekosea kuskiliza maneno ya watu na akaniambia rafiki yangu alimtongoza baada ya sisi kuachana, sikuamini.
Lakini pia nikaja kugundua kuwa yule rafiki angu amenigombanisha sana na watu. Mimi nilikuwa introvert ila yeye ni extrovert anaongea na kila mtu, akawa anajitahidi kunichafua kuwaambia watu namnyanyasa, nampelekesha, nina roho mbaya na ninaringa. Hichi kitu kimeniathiri sana hadi leo sitaki urafiki wa ovyo na mtu.
Wewe nini kilikukuta?