Ni kitu gani kilikufanya ukavutiwa na JF?

Mpandisha mishahara

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2014
Posts
1,742
Reaction score
1,558
Karibuni tukumbushane ni jambo gani lililokushawishi kufungua akaunti JF, na jukwaa gani lilikuvutia zaidi?

Nikianza na mimi, nilifungua akaunti JF baada ya kupendelea kugoogle baadhi ya mambo, mwishowe majibu mengi nayoyapata kupitia link ni kutoka JF. Nikaona isiwe tabu, niwe member kabisa.

Tuhabarishane hapa.
 
JF ni platform ya wazee, mi nliingia tu kusoma habari niliona Instagram page ya JF walipost. Kuingia huku wanaleta mambo ya ooh don't have an account?, nkaona isiwe kesi nikasign up tu, ila siifeel JF huku kila mtu ana hasira, chuki, majungu, ushamba na uzamani, mtu mwenye roho njema na hakwazi watu ni Mshanajr wengine wote chenga tu.
 
Hahahah mkuu umeamua kutoa ya moyoni. Je, uliwahi kuomba ushauri wowote na hukupata msaada humu JF kutoka kwa members tofauti na mshana jr?
 
Hahahah mkuu umeamua kutoa ya moyoni, je uliwahi kuomba ushauri wowote na hukupata msaada humu jf kutoka kwa members tofauti na mshana jr?
Hahah hamna mkuu, mshana ni sample tu, wapo wengi wa aina yake, kuna ushimen , nk nk ila kuna wengine mzee ni wakata kamba mtu lbda anaomba ushauri, wanaanza kumponda tena, inakeraga kweli. Ila labda ni kwasababu huku tunaficha ID zetu ndiYo maana watu wanajibu ovyo hawajali kitu.
 
Mi binafsi JF naifananisha na kijiji, nadhani ndio maana ikaitwa Jamii, katika jamii kuna watu wa kila aina. Ukiomba ushauri wapo watokejeli pia wapo wataokushauri na kuguswa na jambo lako.

Lakini uzuri wa JF kila Jukwaa kuna watu wake; Mfano, unakuta mtu jukwaa la mapenzi yupo, lakini ukienda jukwaa la siasa hajawahi kupitia chochote. JF tamu bwana!
 
one of my friend alinidokezea hii forum,.ilikua 2014 but nikawa nafatilia bila kujiunga rasmi,

kilichonivutia zaidi ni discusion of ideas ambazo zina mvuto, hazichoki kusoma na threads ni nyingi, unaamua usome ipi,
hasa comments za wadau after thread, i liked that.
 
Wewe ni kama Mimi.. Nilianza kuifatilia jf 2011, nikaja kujisajili 2014 mwanzoni
 

Mshana Jr made me join Jamii Forums.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…