Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,637
- 47,413
Kwa upande wangu kuna kipindi nilisafiri kwa siku kadhaa, nikiwa huko nikapigiwa simu kwamba wezi wamevunja dirisha ghetto kwangu na kuniibia. Ikabidi nikatishe shughuli zilizonipeleka kule na kuamua kurudi niangalie mazingira. Hawakuchukua vitu vyote, ila vilivyobaki navyo viliharibika (nadhani katika purukushani ya kuvibeba). Kati ya vitu walivyoiba, kulikuwa na vitu ambavyo ndio nilikuwa navitumia kwenye biashara zangu za wakati huo. Kiufupi wakawa wamenirudisha nyuma sana.
Nilimpa taarifa aliyekuwa mpenzi wangu, kwavile hakuwa anaishi mbali na pale, akaja hadi eneo la tukio. Akanipa pole, tukaenda wote polisi kureport tukio. Wakati ananiaga arudi kwao, akaniambia anashida ya kiasi fulani cha hela maana Mzee wake anaumwa. Sikuwa vizuri kifedha muda ule maana ndio nimetoka safari, alaf pia biashara ndio kama hivyo nishapigwa tukio. Hivyo nikamwambia kiasi alichoomba kwa muda ule sina, ila avumilie kama siku mbili hivi nione naweza kumsaidia kiasi gani.
Hapo ikawa ugomvi, akalalamika kwamba sijali matatizo yake, siyatimizi kwa wakati, siwapi uzito ndugu zake nk. Akaondoka kwa hasira, hata nauli niliyotaka kumpa akaikataa.
Alinighost for two days, hapokei simu wala kujibu msg zangu
Pale ndio nikapata red flag, kwamba "She doesn't take no for an answer". Jambo ambalo in long run lazima lingetugombanisha tena mara kwa mara. Maana hiyo ilikuwa ni kama mara ya tatu hali hiyo inajitokeza.
From there nikaona tunapotezeana muda, nikamuacha mpaka hasira zake zilivyoisha. Siku aliyoamua kunitafuta, nikamuomba tuonane, akagoma na kusema nieleze shida yangu kwa simu. Sasa sijui alihisi namuita aje kunipa shoo au vipi. Nikamuelezea kwa simu nilichoamua, akajifanya kupanick, haukupita muda ghafla nashangaa mtu huyu hapa mlangoni kwangu. Akawa hataki habari za kuachana ila msimamo wangu ukawa ni huo.
Mwisho wa siku akakubaliana na hali.