Ni kitu gani kilikufanya utambue uliyenae kwenye mahusiano sio mtu sahihi kwako?

Ni kitu gani kilikufanya utambue uliyenae kwenye mahusiano sio mtu sahihi kwako?

Alikuwa anajidai msafi sana.. Kila mara akija #ghetto# lazima abadilishe mashuka... Anakaa hata 3 days ni kubadili shuka tu ila hafui... Yeye anakuta safi nimezifua yeye ni kutandika safi tu.

Akifua sana sana ni soksi zangu tu na leso... Nikaona hapa sio ishu.. Kama kufua hataki kwanini abadili shuka!?... Nikavua kiatu.. Nikasonga mbele kama injili..
🤣🤣🤣🤣🤣🤣mbona sababu nyepesi Sana mkuu.Ila umenichekesha
 
Huwa sijiulizi mara 2 kumpiga chini demu anayeninunia kwa sababu ya kutompa hela. Tena hufurahi sana hiyo "taraka"
Nina nidhamu sana ya hela kwenye mapenzi, kwa sababu mimi sio source of income ya mwanamke.

Yule demu nilikuwa nampa pesa ndogo ndogo, kwa mara moja haizidi 30k. Siku moja akiwa kifuani kwangu akaniambia hata sijawahi kumsaidia jambo kubwa zaidi ya pesa ndogo ndogo.

Baada ya kuondoka, sikupokea tena simu yake. Akatuma watu kuomba msamaha, sikuwajibu.

Mwanamke ukimshamla asikuendeshe
Mwasibu hutaki mzaha kwenye maokoto
 
Alinicall akihitaji niende mahali alipo, long time hatukua tume meet,nilifika right time,tukapga story za hapa na pale,tukalala.....
Alinitumia the whole night,and morning tukaagana nikaondoka....hakunipa hata nauli ya kurudi nilipotoka,

kumbuka usiku huo hakuninunulia hata maji ya kunywa YAANI nili lala na njaa,na asubuh niliondoka na njaa na sikupewa hata shilingi 500.

KATIKA SIKU NAZILAANI KATIKA MAISHA YABGU NI SIKU HII, MWAMBIE HUYU WA USICHANA WANGU NILIMPEA ZAWADI YA BIKIRA YANGU,NILIMPENDA AKIWA HANA KITU MPAKA AKAWA NA KITU.......

MIMI NA YEYE ULE ULIKUA MWISHO WETU, NINAMCHUKIA KUTOKA NDANI YA MOYO WANGU
Kwanini hukumuambia una njaa? Au kwanini haukumpa hela akakuletee chakula hadi ukubali kulala na njaa?
 
Nikiisema yule mngese lazima atajijua tu kama yupo humu

Manake ni kitu cha pekee nimeona kwake tangu nianze game ya mapenzi

Wanaosema duniani hakuna jipya kwa yule mwanaume niliona jipya 🙌
 
Yule wa kwangu alikuwa hajui kumenya machungwa. Yani akimenya lazima ayachimbe chimbe kiasi kwamba huyali kwa raha. Kuna siku walikuja washkaji ghetto, baada ya msosi akatuandalia machungwa. Aisee aliyachimba balaa, nikajiuliza what if wangekuwa wageni wa heshima, si ataniaibisha huyu?

Nikapiga chini.
 
Back
Top Bottom