1. Ni ukatili kumuamsha mtoto saa 10 kisa shule. Okoa huyo mtoto unayemlea.
2. Mtoto anafaulu Kwa wastani wa 'B', mwalimu lazima aandike 'very good'. Kumbuka, A - Excellent, B - Very Good, C - Good na D - Poor/Weak. Si suala la nafasi ya dogo darasani, ni personal progress yake.
3. Wazazi wa Tanzania AMKENI, mmezubaa sana. Kwanini mmeacha shule za binafsi ziwafanye zinavyotaka?
Mzazi una jukumu la kulinda ustawi na maendeleo ya mwanao. Usikubali tu kila linalotoka shule.
- Usilazimishwe kumuweka mtoto boarding
- Mtoto asilazimishwe kufanya homework za kupindukia. Kataza.
- Remedials ni option, si lazima.
- Hoji kuhusu michango na mipango ya shule kuhusu taaluma ya mwanao.