FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
Habari!
Kumekuwa na sintofahamu hivi sasa nisemapo maneno haya hasa katika ukanda wa rasi ya Korea ambapo Korea Kaskazini imeendeleza wimbi la vitisho kwa jirani zake na hivi karibuni imetishia kuzitumia silaha zake za nyuklia endapo kutaibuka mashambulizi dhidi yake.
Wakati hayo yakiendelea, Japan imevipokea vitisho hivyo kwa mtazamo tofauti na kutilia shaka afya ya kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un kutokana na purukushani zinazoendelea nchini Korea Kaskazini.
Kulingana na kauli ya Waziri wa Ulinzi wa Japan Taro Kono, kumekuwepo mienendo ya kutilia shaka nchini humo juu ya afya ya kiongozi huyo wa taifa la Korea Kaskazini hasa katika kipindi hiki cha janga la virusi vya corona linaloikabili nchi hiyo.
Waziri anasema,
"Recent movement in North Korea is quite strange. We suspect COVID-19 is spreading around North Korea and Kim Jong-un is trying not to get infected, so sometimes he doesn’t come out in public. We have some suspicion about his health.”
Kumekuwa na tetesi za hapa na pale kuhusiana na afya ya Bw Kim Jong-un, baadhi wakisema kuwa ni mgonjwa sana huku wengine wakienda mbali na kudai kuwepo kwa mgogoro wa kimadaraka kati yake na dada yake.
Ni kitu gani kinachoendelea ndani ya Korea Kaskazini?