Ni kitu gani kitawafanya watanzania kuondoa uoga na kuungana kuukataa uongozi wa CCM?

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Watanzania bado tunaogopa.

Zaidi ya miaka 60 tumewaamini, tumewavumilia, na tumewapa mamlaka ya kutuongoza. Lakini mpaka leo hali za maisha ni ngumu, ufisadi umetamalaki, rushwa imekuwa mfumo wa maisha, vijana hawana ajira, huduma za jamii ni dhaifu huku wakizidi kujiongezea mishahara na posho kubwa kana kwamba hawapo kwenye nchi hi

Tunalia kuhusu mfumuko wa bei, lakini tunaogopa kuuliza. Tunaona ufisadi kila siku, lakini tunaogopa kusema.
Ajira zimekuwa ngumu kwa vijana lakini tunaogopa kupaza sauti. Tunachekwa na hata kuitwa majina ya fedhea lakini tunaogopa kujitetea.

Watu wanapotea, wanakamatwa, wanatishwa, si kwa sababu wamefanya kosa, bali kwa sababu waliuliza maswali ambayo sisi tunaogopa kuuliza.

Wanaotutawala wanatujua ni waoga:
  • waoga wa virungu (defenda moja kila mtu na njia yake)
  • Waoga wa kupoteza kazi au biashara.
  • Waoga wa kuitwa mpinzani.
  • Woga wa kusema ukweli.
Na hiyo ndiyo silaha yao kuu, wanajua tunaogopa.

Mpaka lini tutakubali kunyanyaswa kwasababu ya woga wetu ?

Sauti ya woga ni kifo cha matumaini. Sauti ya ukweli ni mwanzo wa ukombozi.

Wanaharakati wanajitahidi kuamsha raia lakini raia ni waoga, ni shughuli pevu !!, inakuwa ngumu hata kwa mashirika ya umoja wa mataifa kuingilia kati wakiona hakuna msukumo wa wananchi kiujumla.
 
Sasa hao chadema hata umoja tu ndani ya chama hakuna chauma wapo na ubwabwa vyama vya siasa Tanzania vipo kifala sana

USSR
 
Wengi wenu mnapenda mteremko Yaani vya bure na wizi, Rushwa na mengi tu

Utamuaminisha vipi mtu anaefurahia kofia au hongo ya elfu 2
 
Siku zote raia ndio hufanya maamuzi ya mwisho, hata mitandaoni ukosoaji uwe mkubwa kiasi gani, kama raia hawataingia kwa ground huwa hakuna kinachotokea...

Hata mashirika ya haki za kibinadamu, mashirika ya umoja wa mataifa huwa wanapata nguvu kuingilia kati wakiona kuna msukumo wa raia wenyewe, sio mwanaharakati mmoja mmoja.

Wanaharakati wanajitahidi kuamsha raia lakini raia wamelala.
 
Kuna kipindi huwa naona hata Mbowe aliona kazi anayofanya ni ngumu sana akaona alambe tu asali, wanaharakati wana asilimia kama 30% ya mageuzi lakini raia kwa ujumla wana 70%
 
Sasa hao chadema hata umoja tu ndani ya chama hakuna chauma wapo na ubwabwa vyama vya siasa Tanzania vipo kifala sana

USSR
Kwa hiyo polepole anaesema utaratibu haujafuatwa ni Chadema au Malisa maelewano yao yakoje na CCM polepole akitaka kuongea mnazima mitandao hakuna chama ambacho kinaweza kukamilika kwa 100% tuliza pumbu CCM kuna kesi mahakamani
 
Watanzania bado tunaogopa.

Zaidi ya miaka 60 tumewaamini, tumewavumilia, na tumewapa mamlaka ya kutuongoza. Lakini mpaka leo hali za maisha ni ngumu, ufisadi umetamalaki, rushwa imekuwa mfumo wa maisha, vijana hawana ajira, huduma za jamii ni dhaifu huku wakizidi kujiongezea mishahara na posho kubwa kana kwamba hawapo kwenye nchi hi

Tunalia kuhusu mfumuko wa bei, lakini tunaogopa kuuliza.
Tunaona ufisadi kila siku, lakini tunaogopa kusema.
Ajira zimekuwa ngumu kwa vijana lakini tunaogopa kupaza sauti
Tunachekwa na hata kuitwa majina ya fedhea lakini tunaogopa kujitetea

Watu wanapotea, wanakamatwa, wanatishwa, si kwa sababu wamefanya kosa, bali kwa sababu waliuliza maswali ambayo sisi tunaogopa kuuliza.

Wanaotutawala wanatujua ni waoga:

  • waoga wa virungu (defenda moja kila mtu na njia yake)
  • Waoga wa kupoteza kazi au biashara.
  • Waoga wa kuitwa mpinzani.
  • Woga wa kusema ukweli.

Na hiyo ndiyo silaha yao kuu, wanajua tunaogopa.

Mpaka lini tutakubali kunyanyaswa kwasababu ya woga wetu ?

Sauti ya woga ni kifo cha matumaini. Sauti ya ukweli ni mwanzo wa ukombozi.

Wanaharakati wanajitahidi kuamsha raia lakini raia ni waoga, ni shughuli pevu !!, inakuwa ngumu hata kwa mashirika ya umoja wa mataifa kuingilia kati wakiona hakuna msukumo wa wananchi kiujumla.
gentleman,
CCM inaweza kuitawala Tanzania hadi miaka elfu1 ijayo 🐒
 
Kuna kipindi huwa naona hata Mbowe aliona kazi anayofanya ni ngumu sana akaona alambe tu asali, wanaharakati wana asilimia kama 30% ya mageuzi lakini raia kwa ujumla wana 70%
Ukipita mitandaoni huku utasema serikali inapinduliwa kesho, ukiingia mtaani watu hawana habari , vijiweni mazungumzo ni simba na yanga na bongo flavor..

Inasikitisha sana. Hapo lazima mwanaharakati aone kabisa asali inamuhusu...
 
Shida ni mvua zinanyesha na michicha inajiotea hovyo tu, mtu akishafukia ugali na mchicha akashiba na akaenda korongoni kunywa maji , nikulala na kujamba tu.
 
ukijikita na shuhuli za kiuchumi ndugu wala chama cha mapinduzi hakina shida yoyote zadi sana utatamani kidumu milele
 
Waambie yale majamaa Kule Munduli na Ngerengere yatusaidie kututolea hili balaa nchini mwetu
Sie pekee hatuweziii
 
Back
Top Bottom