Ni kitu gani mzazi/ mlezi alikukosea ukiwa mdogo bila kukuomba msamaha na kinakuumiza mpaka leo, mlioweza kusamehe mlifanyaje?

Ni kitu gani mzazi/ mlezi alikukosea ukiwa mdogo bila kukuomba msamaha na kinakuumiza mpaka leo, mlioweza kusamehe mlifanyaje?

Hakuna mzazi duniani anaomba mambo mabaya kwa mtoto wake ,hata akikuchagulia mke au mme lengo lake huwa ni zuri sana,na kumbuka Akitoka Mungu wa pili ni mzazi hasa mama.Usikumbuke negative kwa mzazi,jitahidi sana ukumbuke negatively kwa mzazi

Wapo wazazi Wabaya Mkuu.
Kusema hakuna ni kijidanganya na kutotumia akili vyema.

1. Wapo wababa wanaobaka mabinti zao.
2. Wapo wazazi wanaowatoa watoto wao kafara Kwa sababu Fulani Ile iwe Uchawi au ushirikina.
3. Wapo wazazi wachawi wanaologa watoto wao wasifanikiwe.
4. Wapo wazazi wanaotelekeza watoto wao na wengi kufikia hatua kuwaua kabisa.
5. Wapo Wamama wanaoingilia maisha ya ndoa za watoto wao.
HAO wote ni wazazi Wabaya.
Na ukitaka ushahidi nitakupatia.

6. Wapo wazazi ambao huwapenda watoto waliofanikiwa huku akiwatenga watoto walioshindwa kwenye maisha.
 
Ila malezi ya kiafrica yaan hutakiwi kujielezea,ukipigwa usilie ukilia unapigwa,kufokewa bila kosa ,kufukuzwa fukuzwa.

Unakuwa muoga muoga tu mliokua mkalelewa na baba na mama mshukuruni Mungu.

Sis wengine tulolelewa kw andugu eheeeee tulikipata.

Ndugu hawawezi kukulea kama wazazi wako

Wengine upendo wa kinafiki hatuna,
Mzazi akizingua tunamzingua,
Mzazi Kama hatupendi nasi hatumpendi
 
Back
Top Bottom