Babu Kijiwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2010
- 4,830
- 4,729
Baadhi ya vitu nilivyo danganywa ni:
1. Kifimbo chake akikiweka chini hakuna anayeweza kukinyanyua hata waje watu 50 hawawezi.
2. Alikuwa na kibuyu cha maziwa fresh ambacho aliambiwa siku yakiganda itakuwa mwisho wa maisha yake hivyo mara kwamara alikua anaenda Butiama kuchungulia kama yameanza kuganda au la.
3. Siku 1 wazungu walikuja wakataka kusafiri naye kwenda Ulaya, sasa mzee Kawawa na Mzee Mwinyi wakang'ang'ania kwenda naye, wazungu wakakataa basi akawaambia wazungu kuwa atakaa mwisho wa uwanja, ndege ikianza kupaa atarukia kwenye tairi na kuwaacha kwenye mataa wenzake.
Basi bwana, wazungu wakakubali akaenda kukaa karibu na mwisho wa uwanja, Kawawa na Mwinyi wakamfuata ndege ikaja kwa speed ilivyoanza kupaa Nyerere akarukia kwenye tairi, bila kuchelewa Mwinyi akadaka mguu wa Nyerere na Kawawa akadaka mguu wa Mwinyi, wote watatu wakawa angani.
Mzee Nyerere akahisi hawa jamaa wanamlemea kwa uzito ikabidi atumie akili akawaambia "CCM HOYE" Kawawa na Mwinyi wakainua mikono yao hewani wakajibu "HOYE" wakajikuta ardhini Nyerere akasepa mwenyewe.
Wewe ulidanganywa nini?
Sent using Jamii Forums mobile app