Nevergive up
JF-Expert Member
- Dec 24, 2024
- 600
- 945
Tuambie changamoto ulizopitia ili tujifunze, je ulitoa pesa, ngono, uchawa, ulienda kwa mganga,au ulipitianini? Mimi bado natafuta job
Hahahahaha ila angalau mkuu kwako hali si mbayaMpka nifike 80 ndio nitasema now bado natafuta tu
Sio mbaya ndio , ila hali kuwa mbaya na kuwa nzuri ni mtizamo tuHahahahaha ila angalau mkuu kwako hali si mbaya
Kilikukuta nini mkuu?Niliwahi kuwa na mahusiano na single mother fulani 🙌 guys nimejionea, siwashauri muwe na mahusiano na hao watu
Daaah pole mkuu.lkn vipi nowKipindi flani nadhani mwaka 2022 Kama sikosei niliacha kazi kwenye kiwanda flani hivi nikasema ngoja na Mimi nikajiajiri
Aisee nilichokutana nacho Sina hamu
Picha linaanza nimechukua sendo za kike na za kiume Basi nikatafuta kijiwe kwenye muingiliano wa watu nikamwaga hapo ajabu ni kuwa wateja walikuwa wanakuja wanachagua Kisha wanaondoka anakuja anachagua Kisha anaondoka
Huwezi amini wiki ilikatika nimeuza pea moja ya kiatu na hapo faida ni Kati ya elfu mbili au tatu na hapo natakiwa nile na nipate mahitaji mengine
Nimekaa pale nikawaza nikasema hapana hapa nitakuja nife njaa
Nikaamua kutoka pale kijiweni mzigo nikauweka ndani
Nikaingia kutafuta vibarua ajabu ni kuwa kila napoulizia kazi naambiwa kazi hamna na hapo Sina hela Basi kichwa kikazidi kupata Moto
Nakumbuka nilikuwa naamka saa kumi na mbili asubuh kwenda kutafuta kazi ikafikia hatua kazi ya kutafuta kazi ikawa ndo kazi yangu
Wakuu hakuna Hali inaumiza Kama unaamka hujui uelekee wapi na huna hela isikie tu kwa mwenzio
Kwa baadae sana nilikuja kupata saidia fundi nikajishikiza pale Ila wakuu mtaani sio poa kabisa
Kwa sahivi Mambo sio mabaya sana Ila nimeweza kujichanga changa nikafungua kaduka kakiaina na Maisha yanasongaDaaah pole mkuu.lkn vipi now
Ulidanganywa na threads za wana JF sio kuhusu kuacha kazi na kujiajiri?Kipindi flani nadhani mwaka 2022 Kama sikosei niliacha kazi kwenye kiwanda flani hivi nikasema ngoja na Mimi nikajiajiri
Aisee nilichokutana nacho Sina hamu
Picha linaanza nimechukua sendo za kike na za kiume Basi nikatafuta kijiwe kwenye muingiliano wa watu nikamwaga hapo ajabu ni kuwa wateja walikuwa wanakuja wanachagua Kisha wanaondoka anakuja anachagua Kisha anaondoka
Huwezi amini wiki ilikatika nimeuza pea moja ya kiatu na hapo faida ni Kati ya elfu mbili au tatu na hapo natakiwa nile na nipate mahitaji mengine
Nimekaa pale nikawaza nikasema hapana hapa nitakuja nife njaa
Nikaamua kutoka pale kijiweni mzigo nikauweka ndani
Nikaingia kutafuta vibarua ajabu ni kuwa kila napoulizia kazi naambiwa kazi hamna na hapo Sina hela Basi kichwa kikazidi kupata Moto
Nakumbuka nilikuwa naamka saa kumi na mbili asubuh kwenda kutafuta kazi ikafikia hatua kazi ya kutafuta kazi ikawa ndo kazi yangu
Wakuu hakuna Hali inaumiza Kama unaamka hujui uelekee wapi na huna hela isikie tu kwa mwenzio
Kwa baadae sana nilikuja kupata saidia fundi nikajishikiza pale Ila wakuu mtaani sio poa kabisa
Mkuu bado sijajipata bado naendelea kusambaza CVUngeanza Wewe kutushirikisha mapito yako!
Mkuu kumbe ww ni mwajiriwa? Vipi madafu uliuza wakati gani?Ulidanganywa na threads za wana JF sio kuhusu kuacha kazi na kujiajiri?
Binafsi hakuna watu ninaowaheshimu kama watu waliojiajiri na kujishughulisha na mishe zao mitaani.
Mi binafsi namshukuru Mungu sijapambana na "street hustle" kwani mara baada ya kumaliza degree 2001 nilipata kazi private sector then 2006 nikaingia serikalini.
Kuna jamaa yangu mmoja nilimuambia tuingie serikalini kipindi hiko akanicheka kuwa naenda kupoteza muda yeye anapambana na private sector. Bwana we, likatokea la kutokea wakaterminate mkataba naye huko private.
Jamaa alikaa miaka 3 bila ajira na anapitia kipindi kigumu sema mkewe alikuwa teacher akawa anamuweka mjini. Jamaa alipigika hadi alikonda na ulikuwa ukiongea naye unaona kabisa jamaa ameathirika kisaikolojia na mbaya zaidi hakuwa na mradi wa kumuingizia kipato nje ya utaalamu wake.
Marafiki zake wengi waliokuwa anafanya nao kazi huko Private hawakuwa wanapokea simu zake na hawakuwa wanampa mchongo wowote. Kila akitumia maombi anakosa kwa kipindi cha miaka hiyo 3. Kuna kipindi majuto yakawa makubwa kwake na ilitokea ajira ya mikataba ya miezi 6 kwenye taasisi nifanyayo akaomba tumuunganishe nayo akakosa.
Ashukuriwe Mungu akapata Provate Moja huko Iringa na hadi sasa anapambama huko.
Usidanganywe kuacha kazi kabla hujapata kazi ya kufanya ambayo itakusaidia ukiwa nje ya kazi.
Pole kwa uliyoyapitia bosi.
Hata sasa nauza tu madafu bro.Mkuu kumbe ww ni mwajiriwa? Vipi madafu uliuza wakati gani?
Inasikitisha sana mkuuKilikukuta nini mkuu?
Kwamba nilishauriwa na Wana jf sidhani Kama haya madai Yana ukweli wowote kwa sababu hiyo 2022 nilikuwa sijui Kama Kuna kitu kinaitwa jfUlidanganywa na threads za wana JF sio kuhusu kuacha kazi na kujiajiri?
Binafsi hakuna watu ninaowaheshimu kama watu waliojiajiri na kujishughulisha na mishe zao mitaani.
Mi binafsi namshukuru Mungu sijapambana na "street hustle" kwani mara baada ya kumaliza degree 2001 nilipata kazi private sector then 2006 nikaingia serikalini.
Kuna jamaa yangu mmoja nilimuambia tuingie serikalini kipindi hiko akanicheka kuwa naenda kupoteza muda yeye anapambana na private sector. Bwana we, likatokea la kutokea wakaterminate mkataba naye huko private.
Jamaa alikaa miaka 3 bila ajira na anapitia kipindi kigumu sema mkewe alikuwa teacher akawa anamuweka mjini. Jamaa alipigika hadi alikonda na ulikuwa ukiongea naye unaona kabisa jamaa ameathirika kisaikolojia na mbaya zaidi hakuwa na mradi wa kumuingizia kipato nje ya utaalamu wake.
Marafiki zake wengi waliokuwa anafanya nao kazi huko Private hawakuwa wanapokea simu zake na hawakuwa wanampa mchongo wowote. Kila akitumia maombi anakosa kwa kipindi cha miaka hiyo 3. Kuna kipindi majuto yakawa makubwa kwake na ilitokea ajira ya mikataba ya miezi 6 kwenye taasisi nifanyayo akaomba tumuunganishe nayo akakosa.
Ashukuriwe Mungu akapata Provate Moja huko Iringa na hadi sasa anapambama huko.
Usidanganywe kuacha kazi kabla hujapata kazi ya kufanya ambayo itakusaidia ukiwa nje ya kazi.
Pole kwa uliyoyapitia bosi.
Daah we jamaa nimekuinulia mikono🖐️🖐️🖐️✋umejua kunichekeshaOgopa issue ya kutafut kazi.
Unatembea na nauli kamili kila mda unaishika isije ikapotea.