Ni kitu gani ulishawahi kukatazwa na mpenzi wako hadi ukajiuliza hivi huyu ananichukuliaje?

Mimi mchaga wangu tukikaaga sehemu akapita mdada mwenye mitako lazima anishtue tuanze kulitazama na kulijadili [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Ni kitu gani ulishawahi kukatazwa na mpenzi wako hadi ukajiuliza hivi huyu ananichukulia je?
Nlizuiliwa kuvaa kaunda suti na suruali za vitambaa eti nlizigawa zote aisee nikanunua kodrai na cadet, nlizuiliwa pia kuvaa tshirt kazini
 
Alianza kunikataza kusuka baadhi ya mitindo ya nywele akawa anataka nisuke anavyotaka yeye tena ya gharama mbali na uwezo wangu na hajawahi kutoa hata mia ila kulalamika sasa ooh hujapendeza ilibidi usuke mtindo fulani. Nikaja nikanyoa kaja tena umepunguza sana nywele hupendezi[emoji849]

Nilikuja kumuacha na hadi leo hajuagi kwa nini nilimuacha labda kama ana akili sawa sawa atajiongeza ajue wapi alinikera. Alianza kulalamika mbona mwembamba sana anataka niongezeke.Yule umbwa nilimuangaliaaa sikuongea kitu toka pale nilimuacha kimya kimya. Anajiliza liza hadi leo eti kwa nini nilimuacha na sijawahi kumuambia sababu. Alininyanyasa sana kihisia sipendagi hata kumuona.
 
Mimi alinikataza kufanya kazi alinambia niache kazi nimpe muda cz sina muda nae na jali sana kazi kuliko yeye.

Nikajisemea tuu huyu demu kachanganyikiwa nikatupa kule na kuambia mpaka na leo anatuma txt za kuomba msamaha simjibu chochote

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Yaan uache kazi umpe muda na bado anataka umpe hela hizo hela utaziokota? Kuna watu huwa nahisi kama kichwan hawapo sawa.
 
Alikua hajiamini kwako huyoo ungeendelea nae ungekua mtumwa Sana,wako wanaume wa hvyoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…