Ni kitu gani ulishawahi kukatazwa na mpenzi wako hadi ukajiuliza hivi huyu ananichukuliaje?

Ni kitu gani ulishawahi kukatazwa na mpenzi wako hadi ukajiuliza hivi huyu ananichukuliaje?

Alinambia niuze gari yangu il nipate mahari nimuoe(in my mind nkasema hiv huyu mse**) mimi gari ndy my fav nikiwa na stress na drive mbali zinaisha, so kila akiwa anauliza umefikia wapi lile swala namzuga kuwa wateja wote hawafiki bei nayotaka, it was 2017/8
Huyo binti hukumpenda tu, sijaona kosa la huyo binti kukwambia hivo, labda kama alikuwa na mapungufu mengine ya kitabia ambayo siyajui cc2500
 
Mtawaacha wanaume wangapi Leejay49
mpaka tutakapopata mtu stable, mtu awe hana kweli unamvumilia akipata atanipa, asa limtu unaliona kabisa lina hela lakini kutoa mpaka akuzungushee weee me habari kama hizo sitaki bora tuachane yaishe🙌
 
Kuna demu wangu wa kando huwa anapenda kunipangia marafiki wa kuwa nao. Nshamwambia ni ngumu kunizuia kutoongea na rafiki ninaemhitaji.
 
Mimi asee nilikatazwa kusmile kwa mdada yoyote, nisimsifie mdada yoyote akiwa kapendeza na kubwa kuliko muda wote nitakao kuwa free basi yeye atakua pembeni yangu...
Asee niliushindwa mtihani kabisa, ingawa yule mrembo nickname yake ilikua ni "Mishepu"
Kuandamana na mbebez kila sehemu siwezi kuna muda nataka niwe peke yangu asee.
 
Aliniambia eti niache ugoro niwe nakula ganja....mpaka leo napiga ganja fresh tu ila tulishatemana na mbwa yule ..shit
 
Hongera kwa kutunza penzi[emoji28]siiku utashangaa umebamba na girl mwingine midomo inameremeta kwa lipstic[emoji23][emoji23][emoji23]

Tushaachana kitambo ila tu nimebakia na mazoea sipaki lipstick
 
Alinikataza nisivae suruali za kitambaa au cardet na viatu vya kupiga kiwi. Nisiwe nanyoa level moja.

Alitamani niwe navaa t-shirt na jeanz na raba, kichwani niwe nanyoa pembeni naachia kidogo juu, au ikiwezekana niwe nazinyongorota virasta. Ndevu niziachie kama za kina Rick Ross, na niwe naenda gym kujaza body. Hivyo vingine nilishindwa ila alinifanya niwe napiga tizi na mpaka sasa nashukuru mazoezi yamekua sehemu ya maisha yangu. Ingawa mm na yule binti hatukuweza kufika mbali.

Nilichogundua, hawa masista duu wanawaadmire sana hawa mabishoo wanaojiweka namna hiyo (ingawa midomoni wanaonyesha kuwaponda). Kibaya zaidi wengi wao future hawana. Ndio maana wanaishia kua single mothers tu.
Umemalizaaa!!

Thread closed!!
 
Mimi alinikataza nisiwe nasikiliza singeli wala kucheza. Akasahau siku ya kwanza kuniona aliniona nacheza singeli ndio akanipenda[emoji57][emoji57]
Na itakuwa ulikuwa unamwaga uno ndio akapenda
 
Back
Top Bottom