Ni kitu gani unapenda kuhusu Tanzania ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
Actually nchi yetu Tanzania ina changamoto nyingi sana na huenda zikachukua miongo mingi kuzitatua. Tumekuwa tukilalamikia changamoto nyingi za nchi hii huku wengi wakitamani zitatuliwe, na hii inaonesha kwamba watu wengi wanaipenda nchi yao, haijalishi tunatofautiana mitazamo kiasi gani lakini wengi wetu tunaipenda Tanzania
Hata Watanzania walioenda kuishi nje ya nchi bado unaona wanaendelea kufuatilia mambo ya Tanzania kiundani wakiwa nje hukohuko kwa sababu nyumbani ni nyumbani tu, haijalishi utaenda wapi, kuna chance kubwa bado ukabaki na emotional connection na Tanzania

Ukiacha mabaya yote, kitu gani unapenda kuhusu Tanzania?
Binafsi napenda sana
1. Mandhari
Tanzania ina landscape nyingi sana za kuvutia kuanzia milima, bahari, maziwa makubwa na madogo, ardhi zenye rutuba, semi deserts, craters, mbuga za wanyama nk


2. Hali ya hewa
Tanzania hali ya hewa ni nzuri sana, hakuna maeneo yenye joto kali kufikia Middle East wala baridi kali kama Greenland. Joto huwa la kawaida maeneo mengi na hata yale yenye joto kali na baridi hayajawahi kufikia level za hatari
Pia mvua zinanyesha za kutosha

3. Chakula
Tanzania ina chakula cha kutosha halafu ni organic sio vya kiwandani. Vingi ni healthy na bei rahisi.
Madawa kwenye chakula cha Tz labda ni yale yanayopuliziwa kwenye mboga za majani au nyanya ambayo yanawesa kuondolewa kirahisi kwa kuosha na maji mengi

 
Vyote ni vizuri ila kibaya ni kimoja tu, CCM, tumeichoka na ndio cancer ya nchi hii na siku ikiondoka hakuna mtanzania atakayebaki akiwa amekonda, kila mmoja atanenepa.
 
Masiwa na asali..ila wanakula wachache..sisi tunaambulia nyuki๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
 
Kiukweli Mimi Sina kile kitu mnachokiita 'Uzalendo'.

Naomba tusameheane tu.
Najua unaipenda Tanzania, na uzalendo ni ngumu kuuficha. Huenda unasema hivyo kwa sababu tu kuna vitu vinaendelea nchini vinakudissapoint ila kwa kusoma huu uzi wako I can confirm unaipenda Tanzania
Soma hapo ulipoandika "kulikomboa taifa letu"
Kwa nini unataka kuikomboa Tanzania kama huipendi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ