Ni kiumbe gani hapa duniani huishi milele bila kufa?

Kuna viumbe hai na viumbe visivyo hai, viumbe hai vyote vitakufa na viumbe visivyo hai haviwezi kufa maana havina uhai
 
Si vyote vitaondoka kwa mujibu wa uislamu. Kuna baadhi ya viumbe vitabaki.
Na hapo utaona ile dhana ya "kila chenye mwanzo kina mwisho" haikubaliki kwenye uislamu.
Mf. Wa vitakavyo baki ni;
1. Arshi ya Allah.
2. Moto(jahannamu).
3. Pepo(jannah)
Hivi vyote vina mwanzo lakini havina mwisho. Toka viumbwe havijafa wala havitakufa
 
Duh..... sorry ila huu ni upuuzi mkubwa sana. Kwanza kufa hakuitaji Israel wala upumbavu gani huko. Kwa uwezo Mungu roho kutoka wala hakuitaji kiumbe kingine kifanye hiyo kazi hapa ndipo kunapodhihirisha kwamba uwezo wa Mungu una limitations kwa mtazamo wenu...., kudai kwamba kuna malaika wawili wanaotazama matendo yako na kuyaandika.
Nina uhakika kwenye mafundisho kuna uwongo mwingi sana umepenyezwa, tuacheni porojo aisee.
 
naomba uniwekee sukari kidogo kwenye hii chai mkuu.
 
Wewe jamaaa ebu dadavua kidogo

Kuna mtu ana miaka 2014??

Alifanya kosa gan ili namm nilifanye

Kwakweli sipendi kufa kabisa japo siogopi
 
Kwa si wakristo ni karibu wote mnk Mungu atakuja atakuta viumbe hai...anaweza asinikute mimi ila atakuta watu wengine..
 
Immortal jelly fish
Hawa wana "technical/biological" immortality. Kufa wanaweza kufa vizuri, japo mara nyingi ni kupitia predation yaani kuliwa na wanaowawinda na mara nyingine udhaifu. Ila hivyo vitiligo visingekuwepo kabisa, basi hawa wangekuwa na uwezo wa kufikia "absolute immortality"
 
Jibu langu hakuna kiumbe atakaekwepa MAUTI si duniani wala mbinguni wala popote pale..
mbinguni kuna viumbe wanakufa? wakifa wanaenda wapi?..interesting[emoji23]
 
Walio katika kristo Yesu hawatakufa tutakuwa na uzima wa milele!




Source [HASHTAG]#hollyBible[/HASHTAG]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…