Soloma TV Online
Senior Member
- Jun 26, 2023
- 104
- 291
Timu ya soka ya Yanga inakwenda kuandika Historia yake ndani ya jiji la Kigali Rwanda kunako michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika. Iko hivi siku ya kesho Jumamosi ya tarehe 16.9.2023 wageni Yanga watavaana na wenyeji wao El Merrikh katika kusaka nafasi ya kutinga hatua ya Makundi ya michuano hiyo, furaha itaendelea tena ndani ya jiji hilo lenye mvuto wa kipekee barani Afrika siku ya Jumapili ya tarehe 17.9.2023 pale ambapo Mchezaji wao kipenzi Fiston Mayele na Pyramid yake watawavaa washika mitutu wa nchi hiyo APR. Na hapa nikutonye tu kuna uwezekano mkubwa kwa Uongozi wa Yanga kuwanunulia tiketi maelfu ya Mashabiki wao waliojazana nchini humo kwenda kumshuhudia Mayele wao.
NA HII TUNAIITA NI YANGA DHIDI YA EL MERRIKH & APR
NA HII TUNAIITA NI YANGA DHIDI YA EL MERRIKH & APR