Ni kosa gani alilolifanya Aboud Jumbe kustahili 'kifungo cha maisha'?

kwa sasa bado alhaj jumbe yuko mji mwema?
au ameshatangulia mbele ya haki? Na bado yuko kwenye kizuizi cha nyumbani?
Ni muda umepita

Jumbe bado yupo hai.

Miaka ya 2005 alikuwa karibu kila siku ya Ijumaa akivuka pale kwenye pantoni alienda kuswali swala ya Ijumaa upande wa mjini na alikuwa gari yake haikai kwenye foleni.

Mwaka wa 2000 kama sijakosea alikwenda Geita kulikuwa na Jitimai (maswala ya kiislam).

Sasa nashangaa kusikia kuwa yuko kwenye kifungo. eeh!!
 
Uzi safi unafundisha historia kamili ambayo wengi hatuijui. Hapa kuna umuhim wa kujenga tabia ya kujisomea maandiko ya kihistoria pia!

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Ni siasa tu. mwenyezi Mungu azide kampa nguvu.
 
Sidhani kama mzee Jumbe alikurupuka! Naamini alifikia maamuzi aliyofikia kwa kusukumwa na ufahamu wake wa habari yenyewe ya muungano. Hata kama angepewa pesa zote za bajeti ya serikali Tz bado haiwi mbadala wa yeye kuwa huru. Mbona kama kafutwa kabisa miongoni mwa watu waliolitumikia taifa hili? Hasikiki tena!? Hata chembe ya haya hamna? Inasikitisha sana h
 
Anaishi mjimwema alie mponza Shalifu Hamad ndio aliopeleka waraka kwa nyerere kwamba jumbe alitaka kuvunja mungano
 
Habari wakuu,

Naombeni kujuzwa, aliyekuwa Rais wa Zanzibar kipindi hiko, ndugu Aboud Jumbe ambaye yupo Kizuizini mjini Kigamboni kwa takribani miaka 31 kifungo chake alihukumiwa miaka mingapi?

Au ndio cha maisha? Mwenye kujua anaweza atujuze maana Mzee Jumbe amezeeka kweli lakini hakuna hata msamaha mpaka leo.
 
Dah....Naandaa makala kuhusu huyu jamaa nitarudi hapa baadae
 
Tuwaachie wazenji maana alikuwa raisi wao. Mzee Sheini kazi kwako
 
HABARI HIZI ZA UPOTOSHAJI ALIWAHI PIA KUZILETA TUNDU LISSU NA AKAPINGWA HATA NA EDWIN MTEI....

Ni habari za kizushi.... na nadhani hata ile sheria ya mitandao huenda isikuguse......
 
Ndio maana tunataka mabadiliko,inakuwaje mtu anatelekezwa nyumbani kwa miaka yote hiyo kwa matakwa ya mtu fulani?mawazo mhando in action!
 
CCM mnataka kusema mzee Aboud Jumbe Mwinyi hayuko kizuizini????? kwa hiyo amezeeka sana na ni mgonjwa hajiwezi ndio maana miaka yote hiyo hahudhurii sherehe za kitaifa!!!!!

Ee Mwenyezi Mungu tunusuru na balaa la CCM na dhulma zao na shari zao Aamin.
 
Kizuizini ili kuwa uhukumiwi bali unawekwa. Bila kupelekwa mahakamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…