wabara
JF-Expert Member
- Sep 30, 2013
- 1,500
- 706
Kwa hiyo Nyerere alikuwa Interahamwe!!! Mhh
Unahitajia ufafanuzi au bado upo ndia panda kusadiki ama kukanusha..!?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo Nyerere alikuwa Interahamwe!!! Mhh
kwa sasa bado alhaj jumbe yuko mji mwema?
au ameshatangulia mbele ya haki? Na bado yuko kwenye kizuizi cha nyumbani?
Ni muda umepita
Ni siasa tu. mwenyezi Mungu azide kampa nguvu.Mbaya wa Aboud Jumbe si Nyerere, bali ni muungano wa wazenji kadhaa ambao hawakukubaliana na mwenendo wa Jumbe wa kujiweka mbali na muungano baada ya kuona kuwa umuhimu wa nafasi ya makamu wa rais ulikuwa unamweza na nafasi ya waziri mkuu wakati huo, yaani Sokoine. Kwa muda mrefu tangu mwaka 1974 nafasi ya Makamu wa Rais ilikuwa na umuhimu sana ambapo Jumbe alimwakilisha Nyerere katika shughuli mbalimbali za kitaifa na za kimataifa, na vile vile alitoa maamuzi mbalimbali kwa niaba ya Rais. Baada ya Sokoine kung'ara sana katika siasa za Tanzania, nafasi hiyo ya Makamu wa Rais ikawa kama imemezwa na nafasi ya Waziri mkuu, ndipo Jumbe alipojisikia vibaya na kutaka kuondoa Zanzibar kwenye Muungano, na kusababisha machafuko ya kisiasa ya 1983. Hatua hiyo ilipingwa na wazenji kadhaa wakiwemo akina Sharif Hamad, Mzee Thabit Kombo, Brigedia Natepe, na wengineo.
Baada ya nafasi yaje kuchukuliwa na Rais Mwinyi, Mzee yule aliendelea kupewa heshima zote kama rais mstaafu, na nadhani ndiye mtu pekee aliyelipwa na kuhudumiwa sana na watanzania bila kufanya kazi yoyote, kwani tangu mwaka 1983 hadi leo hii ni karibu miaka 30 na bado analipwa na kuhudumiwa kama Rais mstaafu. Sidhani kama kuna kiongozi mweingie aliyewahi kuhudumiwa namna hiyo.
Nadhani kuwa alikuwa kakurupuka sana kwa vile kama angekuwa msikivu kidogo, huenda baada ya Sokine kufariki mwaka 1984, yeye ndiye ambaye angeweza kuchukua nafasi hiyo ya urais baada ya Nyerere kustaafu mwaka 1985; nafasi ambayo baadaye ilichukuliwa na Mwinyi aliyekuwa amemrithi umakamu wa Rais.