Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Kila mtu amalize haja zake chumbani kwake,
Kuna ubaya
Kwa ubaya hakuna ubaya ila ni gharama tu!!!kwa mazingira ya Tanzania kutokuwa na uhakika wa maji 100 percent hakuna siku utaifurahia nyumba yako unless uwe na kisima kwamba maji nyumbani kwako ni permanently hayakosekani.

Mimi nina vyoo viwili ndani na bafu ila changamoto ya maji hata hicho cha master sikitumii zaidi ya kuoga ilibidi kujenga vyoo vingine nje ambapo nayo kwangu ilikuwa ni best plan.
 
Madhara ya skwata haya
 
Kwa nini usiweke tank la kuhifadhia maji?
 
Ni kweli,, vyoo vya ndani bila maji yakutosha ni mtihani [emoji846]
 
Kwa nini usiweke tank la kuhifadhia maji?
Ukiwa na familia mkuu tank hata uwe nazo tatu bado utaziona kama ndoo nne,nina tank mbili moja 2000ltr na lingine 4000ltr na kisima cha kuvunia maji ya mvua ila hayo maji kwa matumizi ya kawaida ya familia kufua nguo za watoto na wote ni wadogo hawajaosha vyombo kufua nguo za wakubwa yasipotumika kwa akili hayakai mwezi.

Naishi Mbezi huko maji Dawasa engineer wanafungua siku wanazotaka wao so yanayopatikana kidogo yasipotumika kwa akili itanitoka siyo chini ya 120K per month budget ya maji tu.
 
Duh pole aisee
 
Ni maeneo yasiyopimwa bila shaka, kama maeneo yamepimwa njia zipo ni sheria, unanunua tu plot, habari ya njia utaiona ktk ramani ya block
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…